Wakala wa
Usajili wa Biashara na Leseni, (BRELA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) yasaini hati ya makubaliano ya utendaji kazi kwa
lengo la kurahisisha na kuharakisha taratibu mbalimbali za kiuchunguzi
bila kuathiri Mamlaka na Mipaka ya kiutendaji kati ya taasisi hizi
mbili.
Hafla
fupi ya utiaji saini ya hati ya makubaliano kati ya BRELA na TAKUKURU
yameongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na
Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni leo tarehe 7
Desemba, 2023 katika ofisi ya makao makuu ya BRELA jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Bw Nyaisa amesema kuwa Makubaliano hayo ni kuona
uchunguzi unaenda kwa wakati na kuhakikisha TAKUKURU wanapata taarifa
zilizo sahihi na mahiri kwa wakati huku tukibainisha changamoto zilizopo
katika utendaji kazi baina ya BRELA na TAKUKURU na kupendekeza kwa
pamoja ufumbuzi wake
“Katika
utekelezaji wa majukumu ya kila siku BRELA imekuwa ikipokea barua si
chini ya sita (6) kwa siku kutoka TAKUKURU zinazohitaji taarifa za
usajili wa kampuni mbalimbali, pia tumekuwa tukipokea wito mbalimbali
zinazowahitaji Maafisa wa BRELA kwa ajili ya mahojiano TAKUKURU pamoja
na kuhudhuria mahakamani kushuhudia taarifa za kumbukumbu hizo” amesema
Bw Nyaisa.
Aidha,
CP. Salum Hamduni ameeleza kuwa Mkataba huu utakaosainiwa unalenga
kutia nguvu na kurasimisha ushirikiano wa taasisi mbili kwa maeneo
yaliyokubaliwa na pande zote ambazo ni kubadilishana taarifa za
kiuchunguzi kati ya taasisi hizi kwa lengo la kupata ushahidi
utakowezesha kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, kuimarisha mfumo na
utaratibu wa Mafunzo kwa watumishi wa BRELA kuhusu dhana ya Rushwa,
madhara yake na namna watumishi hao wanavyoweza kupambana na rushwa
ndani ya BRELA na kushirikiana katika kufanya utafiti na tathmini ya
mifumo ya kiutendaji ndani ya BRELA kwa lengo la kubaini na kuziba
mianya ya rushwa ndani ya BRELA.
“Kwa
kutambua kuwa rushwa ni Adui wa Haki, Utawala wa Sheria, Demokrasia na
Maendeleo, Serikali imedhamiria kupambana na tatizo la rushwa kwa nguvu
zote. Aidha, kwa kutambua kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayawezi
kufanikiwa bila ushiriki wa wadau, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa, kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa Sura ya 329, imekuwa ikishirikisha wadau kwa namna mbalimbali
ikiwemo kuingia nao mikataba ya ushirikiano” amesisitiza CP Hamduni.
CP
Hamduni ameongeza kwa kusema kuwa TAKUKURU itauzingatia mkataba huu
kuwa mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuifikia ndoto (vision) ya Taasisi
inayosema “Tanzania isiyokuwa na rushwa”, kama ambavyo inabainishwa
katika Mpango Mkakati wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa
Mwaka 2022/23 – 2025/26.
Ikumbukwe
kuwa mnamo tarehe 8 hadi 9 Julai, 2022 BRELA na TAKUKURU ilikuwa na
kikao kazi cha pamoja mkoani Morogoro chenye lengo la kupeana elimu ya
kiutendaji ili kuleta mahusiano yenye tija katika kutimiza majukumu na
kupeana taarifa mbalimbali kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.
Kutokana
na hilo ilionekana kuna umuhimu kwa Taasisi hizi kuanzisha utaratibu wa
kuwa na vikao vya pamoja kwa lengo la kupeana elimu na uelewa kuhusu
utendaji kazi wa majukumu ya Taasisi hizi, mafanikio na maboresho katika
utendaji kazi kipekee katika usajili wa kampuni na biashara, utunzaji
wa rekodi na taratibu za kufuata baada ya usajili, kubadilishana uzoefu
pamoja na kubainisha changamoto mbalimbali ili kupata ufumbuzi wa pamoja
kwa manufaa ya Taasisi hizi mbili.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Rashid Hamduni leo Desemba 7, 2023 wamesaini Makubalino ya Ushirikiano (MOU), baina ya Taasisi hizo Ili kuboresha utendaji kazi. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za BRELA jijini, Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Rashid Hamduni leo Desemba 7, 2023 wakikabidhiana hati ya Makubalino ya Ushirikiano (MOU), baina ya Taasisi hizo mara baada ya kuzisaini Ili kuboresha utendaji kazi. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za BRELA jijini, Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Rashid Hamduni leo Desemba 7, 2023 wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya Makubaliano ya Mashirikiano (MOU) baina ya Taasisi hizo yenye lengo la kuboresha utendaji kazi. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za BRELA jijini Dar es Salaa
No comments:
Post a Comment