Na Zuhura Rashidi,Iringa.
UWEPO wa
takwimu sahihi za wenye VVU unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya
mipango mikakati katika uratibu wa miradi ya kupambana na ukimwi
imeelezwa mkoani Iringa jana.
Hayo yalisemwa na Maganga Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk. Mohamedi Mang’ula wakati wa
ziara ya wawakilishi wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa
kukabiliana na ukimwi (PEPFAR), pamoja na Shirika la Marekani la
Maendeleo ya Kimataifa (USAID) hospitalini hapo ili kuangalia huduma
mbalimbali za utoaji tiba kwa wenye VVU zinazofadhiliwa na mfuko huo
kupitia USAID.
Dk Mang’ula alisema hayo muda mfupi baada ya
kukabidhiwa msaada wa kifaa cha kufanyia usajili wa wenye VVU kwa
kutumia mfumo wa alama za vidole kilichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkazi wa
USAID, Bwana Craig Hart akishukuru ufadhili wa USAID uliochangia
uboreshaji wa huduma za afya kwa wenye VVU hospitalini hapo.
“Tunaipongeza
Kampuni ya Deloitte inayoendesha miradi hii inayofadhili na Mfuko wa
PEPFAR katika mkoa wetu kwani imeweza kutusaidia kupata mafanikio
makubwa katika kufikia malengo ya 95;95;95 katika kutambua wenye VVU,
waliotambuliwa kuanza kupata tiba na suala la kufubaza virusi vya
ukimwi”, alisema.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi
wa Mradi wa USAID Afya Yangu Kusini, Dk. Marina Njelekela alisema
wamekuwa na safari ndefu ila yenye mafanikio lukuki katika kutekeleza
miradi inayofadhiliwa na PEPFAR kwa kupitia USAID.
Alisema
misaada inayotolewa na PEPFAR kupitia Shirika la USAID imesainia kuokoa
maisha ya watanzania wengi katika kipindi hiki cha miaka 20 huku
kukishuhudiwa uimarikaji mkubwa wa huduma kwa wenye VVU katika vituo
mbalimbali nchini.
“USAID Afya Yangu Kusini tunasharehekea
miaka 20 kwa kuboresha miradi ya PEPFAR USAID, tukipitia hatua
mbalimbali za kimaendeleo moja ikiwa ni kuwajengea uwezo watoa huduma za
afya katika vituo mbalimbali.
“Tumeboresha ubora wa utoaji
huduma bora za VVU na Kifua Kikuu katika ngazi ya jamii, mwaka 2004
tukiwa na vituo vya kutolewa huduma 33 lakini kwa msaada wa PEPFAR kwa
hadi mwaka 2023 tumeweza kufikisha vituo 676.
“Deloitte pamoja
na washirika wake wa kiufundi wa MDH na T-marc tunajivunia sana
kusimamia miradi inayofadhiliwa na PEPFAR, mwaka 2004 aina ya wagonjwa
tulioanza nao kwa sasa imebadilika kabisa, sasa wapo na furaha na
matumaini, wamewezeshwa, hawajisikii unyanyapaa”, alisema Dk. Marina.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Baraa la Taifa la Watu Wanaoishi na UVVU Tanzania
(NACOPHA), Bwana Deogratius Rutwatwa wanaoendesha mradi wa ‘Hebu
Tuyajenge’ alisema moja ya mikakati ya malengo ya mradi huo ni
kuhakikisha pamoja na mambo mengine watu wenye maambukizi ya VVU
wanatambua hali zao.
Ofisa mtendaji huyo alizungumzia suala la
unyanyapaa kuwa moja ya changamoto inayosababisha watu wengi wenye VVU
kushindwa kujitokeza kupata huduma za upimaji na kuunganishwa kwenye
vituo vya tiba.
“Baadhi ya huduma tunazozitoa ni pamoja na elimu
kwa wenye VVU kuhusu namna bora ya kujzuia maambukizi mapya, kutambua
wenza na watoto wenye VVU hivyo kuwaunganisha kwenye huduma za upimaji
na kutoa usaidizi juu ya matumizi sahihi ya dawa za ARV’s.
“Kwa
namna ya kipekee niupongeze Mfuko wa PEPFAR kupitia USAID kipindi hiki
unapotimiza miaka 20 kwa mafanikio na jitihada zake katika kupambana na
janga la ugonjwa wa ukimwi hapa Tanzania”, alisema. Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID) Bw.
Craig Hart (katikati) akiangalia, wakati mmoja wa wenye VVU akijisajili
katika mfumo wa alama za vidole mara baada ya mkurugenzi huyo kukabidhi
msaada wa kifaa hicho kwa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Mfumo
huo unasaidia kupata takwimu sahihi za wenye VVU, jambo ambalo ni muhimu
katika kufanikisha utoaji wa huduma bora . Hafla hiyo iliyofanyika
mkoani humo jana inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko
wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) unaofadhili miradi ya kupabana
na Ukimwi inayosimamiwa na (USAID)
Mkurugenzi
wa mradi wa USAID Afya yangu kanda ya Kusini unaoendeshwa na Shirika la
Deloitte, Dk Marina Njekela, akielezea utendaji na mafanikio ya mradi
huo katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU katika hafla hiyo Mjini
Iringa jana.
Baadhi ya wanawake waliowezeshwa na Mradi wa Hebu tuyajenge
unaoendeshwa na Shirika la NACOPHA wakishangilia wakati wa ziara ya
wawakilishi wa PEPFAR, USAID wakitembelea katika ofisi za shirika hilo
mjini Iringa jana.Mwakilishi
wa mabinti wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Lucy Michael
Mpwage, aliyezaliwa na maambukizi ya ugonjwa huo akitoa ushuhuda pamoja
na changamoto za unyanyapaa alizokumbana nazo katika vipindi tofauti vya
maisha yake na jinsi huduma za miradi ya USAID inayoendeshwa na Shirika
la Deloitte ilivyookoa maisha yake. Ilikua ni wakati wawakilishi wa
mfuko PEPFAR, USAID, mashirika yanayosimamia utoaji wa huduma kwa wenye
VVU pamoja na waandishi wa wabari wakitembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa
wa Iringa jana, kuangalia mafanikio ya miradi hiyo .
Takwimu sahihi nyenzo muhimu mapambano dhidi ya ukimwi
Share This
Tags
# HABARI MBALIMBALI
Share This
Jiachie Blog
HABARI MBALIMBALI
Labels:
HABARI MBALIMBALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.


No comments:
Post a Comment