* Mwanda asema mwitikio mkubwa wa vijana kujiunga na VETA
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Temeke,DC. Sixtus Mapunda,amewataka wahitimu wa Chuo cha Ufundi stadi VETA Chang'ombe kuhakikisha wanaondoa fikra za kuajiriwa badala yake wametakiwa kujiajiri kutokana na fursa zilizopo ambapo dunia ndio inakwenda huko.
Amesema Suala la ajira ni dunia nzima hivyo kwa wahitimu ni kujijenga katika kwenda kwenye soko la ajira la kujiajiri ambapo huko uwanja wake ni mpana zaidi.
DC Mapunda ametoa maagizo hayo leo jijini Dar Es Salaam Mahafali ya 53 ya wahitimu ngazi ya pili,tatu,na Diploma wa chuo cha ufundi stadi Veta.
Aidha,DC Mapunda amesema ujuzi mkubwa waliopata kutoka chuoni ikawe chachu kwao kwenda kujiajiri.
"Naimani hapa mmepata ujuzi wa kutosha mtoke hapa muende mkajiajiri,mtengeneze miradi ambayo itakuwa chachu ya nyie kuajiri wenzenu"Amesema DC Mapunda.
DC Mapunda amesema kwa miaka mingi veta amekuwa ikotoa wahitimu wazuri ambao wamekuwa mkombozi kwa watanzania.
Katika Hatua nyingine,DC Mapunda amesema halmashauri ya Manispaa inajipanga kuja na mpango wa kuwawezesha wahitimu wa veta kwa kuwapa mitaji.
"Halmashauri ya Temeke kupitia makusanyo ya ndani tunakusanya bilioni 40 kwa mwaka,sheria inataka asilimia 4 ipelekwe kwenye kutoa mikopo kwa makundi maalum ,kwahyo tunataka asilimia hiyo tuweze kuwasaidia wahitimu hawa mitaji ili waweze kujiajiri"Amesema Mapunda,
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Chang'ombe,Mhandisi Joseph Mwanda,amesema Chuo cha VETA kimekua tofauti na awali ambapo sasa kinawanafunzi zaidi ya 6000.
"Licha chuo kukua changamoto kubwa ni kupata ajira kwa wahitimu wetu maana idadi ya wahitimu wamekuwa wengi na nafasi ni chache"Amesema Mhandisi Joseph.
Rais Mstaafu wa Chuo cha VETA Chang'ombe,Meshack Mahandu ,akisoma Risala ya wanafunzi wenzake,amesema wanafunzi wamekuwa wakipata changamoto ya kupata mafunzo kwa vitendo,kukosekana kwa uwanja wa michezo,pamoja na kuongeza mafunzo yanayotolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akizungumza na wanafunzi na wazazi katika Mahafali ya 53 ya Chuo cha VETA Chang'ombe yaliyoyofanyika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Chang'ombe,Mhandisi Joseph Mwanda akitoa maelezo kuhusiana Chuo hicho katika mahafali ya 53 yaliyofanyika katika viwanja vya VETA ,Chang'ombe
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akipokea moja ya bidhaa kutoka kwa mwalimu wa Maabara Ally Issa katika mahafali ya 53 ya Chuo cha VETA Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali za matukio kwenye mahafali ya 53 ya Chuo cha VETA Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment