JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WATEJA WA BIA KUJISHINDIA PESA TASLIMU KUPITIA KAMPENI YA SBL

Share This

● Shilingi bilioni 1.5 kuzawadiwa kupitia kampeni ya ‘MAOKOTO CHINI YA KIZIBO’

 Wapenzi wa bia sasa wana kila sababu ya kutabasamu wakielekea benki, kutokana na kampeni kabambe ya Serengeti Breweries Limited ambayo itatoa zawadi zenye jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa muda wa miezi 3.

Kampeni iliyopewa jina la “MAOKOTO CHINI YA KIZIBO” itakayowalenga wateja nchni kote, imezinduliwa leo katika ukumbi wa Kitambaa Cheupe Lounge, Sinza jijini Dar es Salaam na inatarajiwa kudumu mpaka mwezi Desemba, 2023. Kampeni hii inatoa fursa kwa kampuni kuwashukuru wateja wake na kuwataka kuendelea kufurahia bidhaa zake.

Kupitia hatua hii, SBL inalenga kuonyesha upendo na shukrani kwa wateja wake waaminifu huku ikiwataka kuendelea kufurahia bia yenye ubora wa hali ya juu. Katika wiki zijazo, SBL inakusudia kuwazawadia wateja wake na ofa za kusisimua, mashindano na zawadi, ikitoa fursa ya kushinda zawadi za kuvutia na kufurahia kumbukumbu za aina yake.

Azkizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa East African Breweries Limited (EABL), Jane Karuku amesema, “Tunajivunia kutoa zawadi za kusisimua ambazo sio tu zitaleta furaha lakini pia kutoa frusa ya kujipatia kipato. Zawadi mbalimbali za kifedha zitanufaisha idadi kubwa ya wateja, hatimaye kuwasaidia watu wengi zaidi kuwa na kipato kwa muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, amesisitiza, “MAOKOTO CHINI YA KIZIBO” inasukumwa na azma ya kuibua hisia za furaha na kusaidia maisha ya wateja wetu, na nia ya kuacha alama muhimu kwa kuleta sababu za kusherekea kila mahali, na kujitolea kwetu kwa namna ya kipekee kusaidia jamii yetu”.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza, ameongezea kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa miezi mitatu wakiwa wameandaa zawadi zenye thamani ya TZS Bilioni 1.5. Amesema, “Tutakuwa tunatoa zawadi za TZS 4M kila wiki na zawadi nyinginezo za papo kwa hapo kila watakapokuwa wananunua bidhaa zetu mbalimbali kama vile Serengeti Premium Lite, Serengeti Premium Lager, Pilsner, Guiness Smooth, na Smirnoff Ice Black”.

William Lyimo, a.k.a. BillNass, mwanamuziki mashuhuri katika Tasnia ya burudani Tanzania na balozi wa kampeni hiyo, amesema, “Nimefurahia dhamira ya SBL katika kuleta furaha na kusaidia maisha ya wateja wake. ‘MAOKOTO CHINI YA KIZIBO’ inaburudisha, hata kwa masharti yake, tayari unaweza kujionea namna ilivyopokelewa vizuri sokoni”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries, Obinna Anyalebechi, akizungusha  kizibo cha chupa kama ishara ya kuzindua rasmi Kampeni ya "Maokoto Ndani Ya Kizibo," akiongozana na Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries, Rispa Hatibu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa East African Breweries Limited, Jane Karuku (wa pili kushoto), Mkuu wa Masoko ya Bia wa SBL, Rhona Namanya (wa tatu kushoto), Balozi wa Kampeni ya Maokoto Ndani Ya Kizibo, Bill Nas, pamoja na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania, Emmanuel Ndaki, mapema wiki hii katika baa ya Kitambaa Cheupe jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad