Na Mwandishi Wetu
TAASISI
ya WAJIBU iliyoanzishwa kwa lengo la kukuza mazingira ya Uwajibikaji na
utawala bora nchini,imeandaa kikao kazi cha siku tatu cha uchambuzi wa
ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2021/22
jijini Dodoma.
Kikao kazi hicho kilichowajumuisha waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali nchini vya kitaifa na vya kijamii pamoja
na wadau kutoka taasisi zisizo za kiserikali kimeanza tarehe 17 mpaka
19 Oktoba,2023.
Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uwezo
Waandishi wa Habari na Wadau kutoka taasisi zisizo za kiserikali
zinazofanya kazi katika ngazi ya Halmashauri kufanya uchambuzi wa
kisekta na kutengeneza brosha kwa ajili ya kuongeza utekelezaji wa
mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za
mwaka 2021/22
Taasisi ya WAJIBU imekuwa ikifanya shughuli
mbalimbali ikiwemo uchambuzi wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa lugha rahisi na rafiki kila mwaka.
TAASISI YA WAJIBU YAANDAA KIKAO KAZI KUCHAMBUA RIPOTI CAG
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment