Na Mwandishi Wetu, Singida
BOHARI
ya Dawa (MSD) imetoa vifaa tiba na dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh.
Milioni 532.4 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Hospitali ya
Wilaya ya Singida, Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Hosptali ya Wilaya ya
Ikungi na Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa ajili
ya kuboresha huduma za matibabu mkoani hapa.
Akizungumza Oktoba
12, 2023 wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwenye hospitali hizo, Meneja
wa MSD Kanda ya kati Dodoma, Bi. Mwanashehe Jumaa alivitaja vifaa tiba
na dawa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kuwa ni vitanda 9
(ICU Beds) vya kisasa pamoja na dawa.
Alisema kwa Hospitali ya
Wilaya ya Singida vifaa vilivyotolewa ni vitanda viwili vya kisasa vya
umeme (ICU Beds), wakati kwa Kituo cha Kituo cha Afya cha Halmashauri ya
Wilaya ya Itigi kikipokea pasi kubwa ya kunyoshea nguo ( Flat iron
industry), vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, mashuka,
magodoro na viti mwendo.
Mwanashehe alisema utoaji wa vifaa hivyo
ni muendelezo wa uboreshaji wa huduma za sekta ya afya mkoani Singida
kwani Machi 15, 2023 MSD ilitoa mashine za kufulia, vifaa vya kinywa na
meno, usingizi na vitanda Hosptali ya Wilaya ya Singida Ilongero.
Baada
ya kukabidhi vifaa hivyo, Wataalam kutoka MSD walitoa maelekezo na
mafunzo kwa wataalam ambao hospitali zao zimenufaika na vifaa hivyo, ili
wavitunze na vidumu muda mrefu kwani Serikali chini ya Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan, imekuwa ikitumia fedha nyingi kuvinunua.
"Serikali
imekuwa ikitumia fedha nyingi kununua vifaa hivi, hivyo ni wajibu wa
watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha vinatunzwa vizuri," alisema
.Mfamasia wa Kanda hiyo na Afisa Huduma kwa Wateja MSD Kanda ya Kati
Dodoma, Michael Mwakuna.
Viongozi wa Hospitali hizo wameishukuru
serikali kupitia MSD kwa kuendelea kuwapatia dawa na vifaa tiba kwa
wakati jambo ambalo limeongeza tija na ufanisi wa kazi katika utoaji
huduma za afya.
Nao Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Singida, Paul Ndeki, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya
ya Singida, Yusuph Kitinya, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itigi, Emmanuel
Mallange, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kahabi
Kimotoli na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Hussein
Sapoko waliahidi kuvitunza na kumshukuru Rais Samia kwa kuendelea
kuboresha huduma za afya mkoani humo.
“Vifaa tulivyopatiwa
vitatusaidia kutoa huduma zetu tunawashukuru Serikali kwa kufanikisha
upatikanaji wa vifaa tiba kupitia MSD hivyo kuhimarisha utoaji wa huduma
bora kwa wananchi.,.” alisema Kitinya.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kahabi Kimotoli alisema wamepokea vitanda
16 na kufikisha idadi ya vitanda 80 na kueleza kuwa mbali ya vifaa
hivyo pia walipokea baadhi ya vifaa vingine vingi kama magodoro,
mashuka, taa za kufanyia uchunguzi, taa ya chumba cha upasuaji na sasa
wapo kwenye mchakato wa kupelekewa mashine itakayosaidia kufanya
operesheni ya mama na mtoto katika jengo ambalo lipo mbioni kukamilika.
."Kwa
ujumla ni idadi kubwa ya vifaa tulivyoletewa na Serikali chini ya mama
yetu kipenzi Rais Samia kupitia MSD." alisema Dk.Kimotoli.
Kwa
upande wake Mganga wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Hussein Sepoko
alisema Rais Samia amewapelekea vifaa tiba vingi vya kisasa na
akaishukuru MSD kwa ushirikiano inayowapa wa kuwapelekea vifaa tiba na
dawa kwa wakati.
Nao Diwani wa Kata ya Ilongero Issa Mwiru na
Diwani wa Kata ya Itigi Mjini, Ally Minja walipongeza Serikali na MSD
kwa kusambaza vifaa tiba na dawa.
“Kwa nafasi ya kipekee
tunaishukuru MSD wamekuwa na ushirikiano mkubwa tunapohitaji vifaa tiba
na dawa wanatuletea kwa wakati hakika wameendelea kufanya maboresho
makubwa katika sekta ya afya ," alisema Mwiru.
Aidha, Mwiru
aliishukuru Serikali kwa kuwaletea watumishi katika hospitali mpya ya
Wilaya ya Singida na kusifia utendaji kazi wao kwa masaa yote wanapokuwa
kazini.
MSD YAFANYA MABORESHO MAKUBWA SEKTA AFYA SINGIDA, YATOA VIFAA TIBA, DAWA ZA MILIONI 532.4
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.


.jpeg)




No comments:
Post a Comment