Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WANAFUNZI
49 wa Shule ya Mikocheni Islamic wamehitimu elimu ya msingi (darasa
saba) huku uongozi wa shule hiyo ukijivunia elimu wanayoitoa ambayo
inawajenga watoto kuwa raia wema kwa taifa la Tanzania sambamba na
kuwajengea nidhamu na heshima.
Wakati mgeni rasmi katika mahafali
hayo ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
(TASAC) Abdi Mkeyenge akitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa jamii
kuhakikisha wanakuwa wasisimizi wa watoto katika kutumia teknolojia
katika kujenga na si kuharibu.
Akizungumza wakati wa mafahali ya
wanafunzi wa shule hiyo ambao wamehitimu elimu ya msingi kwa maana ya
darasa la saba Mkeyenge amesema kwa sasa kumekuwa na matumizi makubwa ya
teknolojia lakini ni vema kwa watoto ikatumika vizuri.
“Teknolojia
si mbaya kwa maana ya asilimia 100 lakini ina uzuri na ubaya wake sasa
inategemea wewe utatumia ili ikuletee faida au hasara.Kwa maana ya faida
ni kweli tutumie teknolojia ituzalishie.
“Kwa mfano siku hizi
unaweza kuipata dunia yote ukiwa kwenye simu yako kiganja chako kwa hiyo
inategemea unatumia kwa ajili ya nini lakini kwa watoto nimesisitiza
wazazi na walezi tutumie teknolojia iwafae watoto sio.
“Kwa maana
umuachie anakuwa huru kutumia kifaa ambacho kina teknolojia na yeye
mwenyewe akajiamualia afanye nini, unaweza kumuachia akatumia lakini
kifaa kiwe na udhibiti na awe na mipaka ya kutumia hicho kifaa anapokuwa
nyumbani, kama luninga uweke mambo ambayo yanaendana na umri wake kama
ni simu awe anatumia katika masomo,”amesema.
Kuhusu malezi
ameipongeza shule hiyo kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele katika
kuwalea watoto wa kimisingi ya kimaadili yakiwemo ya dini , hivyo
amewataka walimu kuendelea na kusimamia maadili lakini na wanafunzi nao
kujivunia utamaduni wa shule hiyo na wajivunie walivyo kokote
watakakokwenda.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mikocheni Islamic
Zuwena Hamis amesema jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu elimu ya msingi
wakiwemo wasichana wakiwa 29 na wavulana 20 huku akieleza namna
wanavyojivunia kutoa wanafunzi walioiva katika masomo ya elimu ya
kimazingira na vitendo.
“Tunajivunia msingi imara wa wanafunzi
ambao tunategemea watakuwa mabalozi wetu na raia wema kwasababu
tumewafundisha maadili kwa vitendo, wameiva kimazingira lakini katika
maadili.
“Tumetoa wanafunzi ambao wako vizuri katika sayansi,
wako vizuri katika vitendo, wako vizuri katika heshima na nidhamu lakini
wameiva katika eneo la imani dini.”
Amefafanua kwa sasa
ulimwengu umebadilika hivyo mwanafunzi anahitaji kulelewa katika
mazingira yote ikiwemo kupewa elimu ya mazingira, elimu ya vitendo na
anahitaji kupewa maadili na malezi mema yanayomuwezesha kumsaidia kuwa
raia bora na kijana bora wa hapo baadae
“Kwa hiyo hili ni jambo
kubwa tunalojivunia kwamba elimu tunayotoa ni kwa njia ya vitendo,
tukimfundisha dini tunafundisha kwa vitendo, kama heshima tunafundisha
kwa vitendo na kama ibada tunafundisha kwa vitendo.Watoto wetu wameiva
katika maeneo yote.”
Akitoa ujumbe kwa wazazi na walezi, amesema
ni vema wakatambua wanapowafundisha wanafunzi wanafundisha vitu ambavyo
viko katika mpangalio lakini wanapofika nyumbani wazazi wamekuwa na
majukumu mengi hivyo hawapati nafasi ya kusimamiwa nyumbani.
“Watoto
wanatumia muda mwingi kuangalia luninga na mitandao mingine ya kijamii
ambayo hawaitumii kwa usahihi.Wanakuwa wanapoteza muda mwingi kwa mambo
yasiyokuwa na faida lakini wazazi hawajui kwa kuwa wanatoa nyumbani
mapema na kurudi usiku.”
Aidha amesema kumekuwa na changamoto ya
mtoto kulelewa na mzazi mmoja aidha baba au mama na hilo ni tatizo kubwa
linaloathiri watoto , hivyo ameshauri wazazi kuangalia hatma ya watoto
wao kwa kuhakikisha wanavumiliana na wanaishi pamoja.
“Wazazi
hawafikirii kwamba ndoa ni kitu cha msingi ambacho baba na mama wakiwa
pamoja malezi ya watoto yanakuwa mazuri .Wanapokuwa mbalimbali watoto
wanaathirika kwa kiwango kikubwa,wanachanganyikiwa kimasomo na wanakosa
mapenzi ya wazazi wote wawili, hivyo ni vema wazazi wakakubaliana ili
kutengeneza familia iliyo bora.”
Wahitimu wa Shule ya Mikocheni Islamic wakitumbuiza wakati wa mahafali hayo
Mwanafunzi Sakina Rashid akisoma rasala yao mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa mahafali hayo .
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania( TASAC) Abdi Mkeyenge
akizungumza wakati wa mahafali hayo ya shule ya Mikocheni Islamic
iliyopo jijini Dar es Salaam.jpeg)
Mwenyekiti
wa bodi ya Wadhamini Shule ya Mikocheni Islamic Alhaj Othman Janguo
akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo
Mwalim
Mkuu wa Shule ya Mikocheni Islamic Zuwena Hamis akizungumza wakati wa
mahafali ya darasa la saba la wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi
mwaka 2023.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Mikocheni Islamic


No comments:
Post a Comment