*Kuanza Oktoba 21 vituo mbadala vyatajwa
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imetoa vituo mbadala kwa basi zilizokuwa zikitumia Kituo cha Kivuko Feri.
Hatua ya kutotumia kituo cha kivukoni ni kutokana na kituo hicho kuanza matengenezo kwa ajili ya miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo hataka awamu ya Nne.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano DART William Gatambi amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza hivi karibuni hivyo Oktoba 21 kutakuwa na utepe ambapo Daladala hazitaingi kupakia wala kushusha abiria katika kituo hicho.
Amesema vituo mbadala ni kituo cha Ardhi kwa mabasi , Kituo cha Uhio na Baharini NBC kwa dalada zilizopangiwa kutokana na barabara zinazotumia.
Gatambi amesema upanuzi wa kituo cha Kivukoni kitatumiwa na mabasi yaendayo haraka pale kitapokamilika daladala hazitaingia.
Afisa Mfawidhi wa LATRA jiji la Dar es Salaam Rahim Kondo amesema kuwa daladala zote zifike katika vituo vilivyopangwa na bila kufanya hivyo watakuwa wamekiuka taratibu za leseni.
Amesema kuwa baadhi ya madereva wa daladala wataanza kushusha sehemu ambazo hawajapangiwa kwa madai ya kuwa hawatakiwi kufika.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam Shufwaya Lema amesema wanakubaliana na maendeleo na kwenda kuwapa taarifa madereva wa Daladala .
Daladala Stop Kituo cha Kivukoni
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.




No comments:
Post a Comment