Kaimu Mkurugenzi Uzingatiaji na utekelezaji wa sheria Baraza la uhifadhi na utunzaji Mazingira Dk. Thobias Mwesiga akimpa maagizo meneja wa Kiwanda Cha Chanzi kinachozalisha Funza
Meneja wa Kiwanda Cha Chanzi kilichopo mkoani Arusha Mayasa Mhina akieleza shughuli zinazofanyika Kiwandani hapo ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa funza kwa ajili ya chakula Cha mifugo
Taka ozo zilizoandaliwa Kwa ajili ya kuanza mchakato wa uzalishaji Funza.
Na Jane Edward, Arusha
NEMC yampa siku Saba mmiliki wa Kiwanda Cha Kuzalisha chakula Cha mifugo Kwa kutumia taka laini kudhibiti harufu Kali itokanayo na taka hizo jambo ambalo limekuwa kero Kwa wakazi waishio eneo linalozunguka Kiwanda hicho.
Agizo hilo limeitolewa na Kaimu Mkurugenzi Uzingatiaji na utekelezaji wa sheria NEMC Dk. Thobias Mwesiga alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo mkoani Arusha ambapo amemtaka mwekezaji huyo kuhakikisha wanatafuta mbinu mbadala wa kuzuia harufu kusambaa na kusababisha kero Kwa wakazi wanaoishi maeneo yanayozunguka Kiwanda hicho.
"Hatuna nia ya kufungia Kiwanda hiki lakini lengo letu tunapaswa kutoa elimu na hivyo basi tulipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi maeneo haya kwamba harufu kali inayosababishwa na shughuli zinazotekelezwa hapa imekuwa kero kwao, hivyo tukatumwa na Waziri anayesimamia Shughuli za Mazingira Ili kuja kutembelea na kukagua shughuli hizo, tumejionea Sasa natoa siku Saba kudhibitiwa Kwa harufu hii"
Lengo la NEMC siyo kuwakwamisha Wawekezaji bali ni kuona mwekezaji ana
tekeleza shughuli zake Kwa kufuata sheria na tumeona kwamba kiwanda hiki kinafanya kazi ya kubadilisha taka laini (muozo) kuwa bidhaa hili ni jambo jema, lakini hatutaki kuona mnatoa tatizo moja sehemu flani na kulihamishia mahali pengine Kuzalisha tatizo jingine, kama mmehamua kufanya hivyo maana yake mje na mbinu mbadala ya kudhibi hii harufu" alisema.
Dk. Mwesiga alisema endapo siku Saba zitatimia Kiwanda hicho kikiwa bado kinalalamikiwa au kushindwa kutimiza sheria na kanuni za Mazingira ni dhahiri kuwa kitachukuliwa hatua Kali ikiwemo kupigwa faini pamoja na kufungiwa kufanya uzalishaji.
Aliitaka halmashauri ya Jiji la Arusha kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa eneo la Mwekezaji huyo Ili aweze kuhamisha Kiwanda hicho na kukipeleka mbali na Makazi ya binadamu Ili kuweza kufanya shughuli zake Kwa uhuru.
Naye Ofisa Mazingira Jiji la Arusha Sigfrid Mbuya alisema tayari mwekezaji huyo alishapeleka Mapendekezo (Proposal) ya kuomba eneo la kujenga Kiwanda kikubwa Kwa kuwa eneo walililopo Kwa Sasa limekuwa dogo na Ili kuondoa kero kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo alisema wataalamu wa Jiji walishapitia mapendekezo hayo na kilichobaki ni kupitishwa kwenye vikao vya Jiji Ili kupatiwa Eneo hilo.
" Waliomba Eneo lililotengwa kwa ajili ya dampo Ili kuendesha shughuli zao Kwa uhuru hivyo tulishapitia mapendekezo hayo na imebaki kupita kwenye vikao vya halmashauri waweze kupatiwa maeneo hayo, lakini pia hiki Kiwanda kinafanya kazi ya kubadili taka jambo ambalo ni teknolojia ya maana, kama Kwa siku zinakusanywa taka zaidi ya tani 100 lakini hapa wanauwezo wa kuchukua taka tani 30 maana yake ni teknolojia ya maana ,hivyo ni namna tu ya kuweza kukamilisha taratibu zinazotakiwa na kuendelea na uzalishaji " alisema.
Naye meneja shamba wa Kiwanda hicho Mayasa Mhina alisema walishafanikiwa kudhibiti harufu hiyo lakini tatizo limejitokeza pindi umeme ulivyoanza kuwa wa mgao.
"Tumefanikiwa Kwa kiwango kikubwa kudhibiti harufu Katika uzalishaji wetu lakini tangu umeme uanze kukatika mara Kwa mara ndipo tatizo lilipoanzia hapo, lakini umeme ukirudi tu kazi ya kuondoa hizi taka inaanza lakini pia Huwa tunatumia vumbi la mkaa kudhibiti harufu"alisema Mhina.
Kiwanda hicho huchakata taka laini na Kuzalisha funza kwa ajili ya kutengeneza chakula Cha mifugo (protein ya mifugo) pamoja na mbolea.
No comments:
Post a Comment