-Mkurugenzi Mkuu abainisha mafanikio lukuki, amesema yamechangiwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
TEF yakoshwa na utendaji wa NSSF yapongeza kazi kubwa inayofanywa
Na MWANDISHI WETU
Ni
funga kazi pengine unaweza kusema hivyo! Baada ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba kubainisha
mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Mfuko katika kipindi cha Machi 2021
hadi kufikia tarehe 30 Juni 2023.
Mshomba amesema hayo tarehe 25
Septemba, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa wasilisho la
utekelezaji wa majukumu ya NSSF kati ya Machi 2021 hadi Juni 2023 kwenye
kikao kazi baina ya Mfuko, wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali
vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).
Amesema
NSSF imefanikiwa kuandikisha wanachama wapya 547,882, kati ya tarehe 1
Machi 2021 na 30 Juni 2023 na kwamba idadi ya wanachama wachangiaji
iliongezeka kwa asilimia 36 kutoka 874,082 tarehe 1 Machi 2021 hadi
kufikia wanachama 1,189,222 tarehe 30 Juni 2023.
“Siri ya
mafanikio hayo kuwa ni pamoja na mkakati wa Serikali ya awamu ya sita
chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, sera nzuri za kuvutia wawekezaji, pamoja na
utekelezaji wa mpango wa Mfuko katika uandikishaji wanachama na matumizi
ya TEHAMA,” amesema.
Kuhusu makusanyo ya michango amesema katika
mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, kwa mwezi yaliongezeka
kutoka shilingi bilioni 97.67 iliyofikiwa tarehe 1 Machi 2021 hadi
kufikia TZS bilioni 143.05 kwa mwezi katika mwaka wa fedha ulioishia
tarehe 30 Juni 2023.
Hata hivyo, amesema makusanyo ya michango
kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 43 hadi kufikia shilingi bilioni
1,718.28 katika mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2023 ukilinganisha na
shilingi bilioni 1,201.05 zilizokusanywa katika mwaka ulioishia tarehe
30 Juni 2021.
Amesema uwekezaji wa Mfuko pia uliongezeka kwa
asilimia 111 kutoka shilingi bilioni 3,395.46 tarehe 1 Machi 2021 hadi
kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023. Kati ya mwaka wa
fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 na mwaka ulioishia tarehe 30 Juni
2023, thamani ya vitega uchumi vya Mfuko imekua kwa asilimia 55 hadi
kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023 kutoka shilingi
bilioni zilizokuwa tarehe 30 Juni 2021.
Mshomba amesema katika
mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, NSSF ilitumia wastani wa
shilingi bilioni 61.93 kwa mwezi kulipa mafao mbalimbali kwa wanachama
na wategemezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 ukilinganisha na wastani
wa shilingi bilioni 50.58 kwa kipindi kilichoishia tarehe 1 Machi 2021.
Aidha,
kati ya mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 na mwaka wa fedha
ulioishia tarehe 30 Juni 2023 malipo ya mafao yaliyolipwa kwa wastaafu,
wanachama na wanufaika wengine yaliongezeka kwa asilimia 25 na kufikia
shilingi bilioni 743.17 katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023
ukilinganisha na bilioni 594.33 zilizolipwa Juni 30, 2021.
Kuhusu
Mpango wa Taifa wa Sekta isiyo Rasmi (NISS), Mshomba amesema Mfuko
umefanya mapitio ya Mpango wa utoaji wa huduma za Hifadhi ya Jamii
katika sekta isiyo rasmi (NISS).
Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF), Deusdatus Balile amepongeza mafanikio
mbalimbali ya NSSF yakiwemo ya ongezeko la michango, ongezeko la
wanachama wachangiaji, ongezeko la mapato pamoja na ulipaji wa mafao.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akizungumza katika kikao kazi
kilichoratibiwa kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana
katika kipindi kilichoanza tarehe 1 Machi 2021 hadi Juni 30, 2023
ambapo amesema NSSF imepata mafanikio kwa upande wa uandikishaji
wanachama, ukusanyaji michango, uwekezaji na kulipa mafao.
Kikao
kazi hicho na wahariri wa vyombo vya habari kimefanyika katika kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam,
tarehe 25 Septemba 2023 chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Wakurugenzi
kutoka Kurugenzi mbalimbali pamoja na baadhi ya Mameneja wa NSSF
wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha
Mshomba (hayupo pichani) na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. Mkutano huo umefanyika
tarehe 25 Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akitoa neno la
utangulizi katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika tarehe 25
Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Matukio katika picha wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili Hazina.
No comments:
Post a Comment