Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea Banda la Benki hiyo,
kujionea shughuli wanazofanya katika maonesho ya Teknolojia ya Madini
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Bomba mbili - EPZ leo Septemba 23,2023,
Mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
GEITA.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa jumla
ya kilo 418 za Dhahabu tayari zimeshafirishwa kwenda nchini Uingereza
kwaajili ya kuisajili kwenye soko la kimataifa na mfuko wa kuhifadhi
dhamana na hifadhi za Kimataifa.
Gavana Tutuba amebainisha hayo
leo Septemba 23, 2023 kwenye Mahojiano na Waandishi wa habari wakati wa
ziara yake fupi ya kutembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya Teknolojia
ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ - Bomba mbili Mkoani
Geita.
Amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania toka ipate Uhuru, Serikali ilikuwa ikitunza fedha za kigeni
ikiwemo Dola lakini sasa imeingia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi
Dhahabu kutoka Tanzania.
"Tayari kwa mara ya kwanza tangu
Tanzania ipate uhuru tulikuwa tunatunza na kuhifadhi fedha za kigeni
ikiwemo Dola, lakini kwa mara ya kwanza sasa imengia kwenye historia ya
nchi zinazo hifadhi dhahabu ambayo imenunuliwa Tanzania,"amesema.
Ameeleza
kuwa wamejipanga kuendelea kununua Dhahabu kwa wachimbaji wadogo,
wakati na wakubwa, pamoja na wauzaji wengine waliopo kwenye maeneo
mbalimbali, na kwamba wanaendelea kuhamasisha wananchi kutembelea banda
la BoT kupata elimu na kufahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu
yao kupitia Benki hiyo.
"Hivi sasa kwenye Maonesho haya
tunaendelea kuhamasisha watu waje kupata elimu na kufahamu namna ambavyo
wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia BOT.
"Kwasababu sisi
tunanunua wenyewe, tunatoa bei halisi ya soko kwa siku hiyo, tofauti na
wengine ambao wamekuwa wakinunua kwa bei za chini, inawezekana isiwape
manufaa makubwa kama wanavyotarajia" ameeleza Gavana Tutuba,
Aidha
amesema kuwepo kwao kwenye maonesho hayo kumetoa fursa kwa wananchi
kufahamu mifumo yao ya kudhibiti uharifu kutokana na uwepo wa wachimbaji
na baadhi ya wadau wa madini kupokea fedha nyingi au kutumia fedha
tasilimu katika miamala yao ya kulipa au kupokea fedha hizo.
kutokana
na changamoto hizo, BoT imetengeneza Mfumo wa kurahisisha unaoitwa
'Tanzania Payment System' (Tips). uliounganishwa mabenki yote na watoa
huduma wa miamala kwa njia ya kampuni za simu.
"Kwa kutumia
mfumo huu, umepunguza gharama za kuhamisha miamala kutoka Kampuni moja
kwenda nyingine au kubadilishana kutoka benki moja kwenda nyingine"
amesema Gavana Tutuba.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili kushoto) akitoa
Maagizo kwa Meneja Msaidizi Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha
za kigeni nchini, Dkt. Anna Lyimo (kulia), alipokuwa katika ziara fupi
ya kutembelea Banda la Benki hiyo, katika Maonesho hayo. (wa kwanza
kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria
Msina.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili
kushoto), akimsikiliza Bw. Ephraim Madembwe, Mchambuzi Mwandamizi
Masuala ya fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya fedha, Benki Kuu ya
Tanzania (BoT). (wa kwanza kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili
kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Mkuu katika
Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo Bi. Kidee Mshihiri (kulia), alipokuwa
akielezea kazi na majukumu yanayotekelezwa na kurugenzi yao. (wa kwanza
kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria
Msina.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (katikati)
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella (kushoto) wakati
Mkuu wa Mkoa huyo alipofika katika Banda la Benki hiyo kukutana na
Gavana pamoja na kujionea namna BoT inavyotekeleza Majukumu yake katika
Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ -
Bomba mbili Mkoani Geita. (kulia), ni
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (katikati),
akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Emmanuel Tutuba, (kushoto),
wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofanya ziara fupi kwenye Banda la Benki
hiyo kwenye Maonesho ya Madini Geita. (kulia), ni Meneja Mawasiliano
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Bw. Martin Shigella, (kushoto), akiagana na Meneja
Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina, (kulia),
mara baada ya kumaliza mazungumzo yake mafupi na Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (katikati), katika Banda hilo.
Baadhi ya watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), katika picha ya pamoja.
(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
GAVANA TUTUBA: DHAHABU YA TANZANIA KUSAJILIWA KWENYE SOKO LA DUNIA LONDON
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment