NA FARIDA MANGUBE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamtafuta Dereva wa Gari namba T904 DKY Kampuni ya Abood kwa kosa la kugonga gari aina ya Noah lenye namba za usajili T828 DNB na kusababisha ajali iliyouwa watu wawili na wengine wawili kujeruhiwa.
Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama ajali hiyo imetokea Tarehe 11.09. 2023 majira ya saa tatu asubuhi barabra kuu ya Dar es Salaam - Morogoro maeneo ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro ambapo chanzo cha ajali matumizi mabaya ya Barabara, Dereva wa Basi alicha upande wake na kutumia upande mwingine na kuigonga Noah.
Scolastica Solomon, Kaim Afisa Uhusiano Hospatali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amesema wamepokea majeruhi wawili waliofahamika kwa majina ya Ally Sarehe na Shabani Salumu Mdango na miili miwili ya marehemu ambapo ammoja amefamika kwa majina ya Safiri Kibwana huku mwingine akiwa bado hajatambulika.
DEREVA WA ABOOD ASAKWA KWA KUSABABISHA AJALI MOROGORO
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.



No comments:
Post a Comment