Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko imefanya ziara ya Ukaguzi wa kikosi cha Mbwa katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikosi hicho katika eneo hilo, kuhakiki ufanisi wake na kuboresha utendaji
Akizungumza na
Maafisa wa Uhifadhi na Askari wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam na Pwani
pamoja na kikosi cha K9 kinachojumuisha Askari Wenye mafunzo maalumu
kwa ajili ya ukaguzi wa nyara za maliasili katika viwanja vya ndege na
bandari Septemba 15, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mej. Jen. (Mstaafu)
Semfuko amewasisitiza wahifadhi hao kuongeza Ubunifu na weledi katika
utekelezaji wa majukumu yao na kuwa na mahusiano mazuri katika shughuli
zao Ili kuzilinda rasilimali za nchi.
"Ninyi ndio waanzilishi na
ndio mtakuwa viongozi wakuu hapo baadae wa Unit hii hivyo TAWA
tunatakiwa kuwa wabunifu wa viwango vya juu” amesema
Nae Naibu
kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mlage Kabange amesema wameridhishwa na kazi
nzuri ya udhibiti na ukaguzi wa nyara zinazotoka na kuingia hapa nchini,
kwahiyo katika eneo la uwanja wa ndege jukumu hili linafanyika vizuri
kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za ulinzi na Usalama katika
kudhibiti wa utoroshaji wa nyara nje ya nchi.
"Mabadiliko haya
chanya hayajaja kwa bahati mbaya, kunasababu ambazo zimefanya tuwe na
mabadiliko makubwa na chanya kama haya ni Uadilifu, Uwajibikaji, Nidhamu
ya hali ya juu, Mikakati na timu work" tunategemea juhudi zaidi na
weledi zaidi katika kutekeleza majukumu yenu, alisema mmoja wa wajumbe
wa bodi Prof. Jafari Kideghesho.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa
Kiwanja Cha Ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere, Lugano Mwansasu
ameeleza mafanikio yanayopatikana katika udhibiti wa nyara za serikali
viwanjani hapo kupitia TAWA.










No comments:
Post a Comment