WIZARA ya Mifugo na Uvuvi kupitia kituo cha Taifa cha Uhimilishaji(NAIC) imefanikiwa kusambaza mbegu bora za mifugo zaidi ya 150,000 kwa wafugaji kote nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa
Kituo hicho Agosti 6,2023, Dk.Dafray Bura katika maonesho ya Kilimo
Mifugo na Uvuvi NanenaneKanda ya Kaskazini yanaoendelea mkoani Arusha
Amesema
mbegu hizo zinazozalishwa na kituo hicho zimeonesha kuleta tija kwa
wafugaji baada ya kutoa matokeo chanya kwa mifugo hiyo kuwa na uwezo wa
kutoa maziwa mengi kuanzia lita 35 hadi 40 kwa ng’ombe mmoja.
“Mbegu
zetu zimeonesha matokea mazuri mfano leo tumefanya paredi ya ng’ombe wa
maziwa kuna ng’ombe alikua anatoa lita 38 hadi 40 kwa mkamuo ambao ni
moja ya matokea yaliyotokana na madume yetu ambayo mbegu zao tumesambaza
kwa wafugaji, ” amesema
Amebainisha kwasasa kituo kina aina tisa
za madume ya mbegu ambapo licha ya kuzalisha mbegu hizo kwa ajili ya
wafugaji pia kituo hicho kinatoa mafunzo kwa watu wanaotaka kufanya kazi
ya uhimilishaji
Amebainisha lengo la Serikali ni kuwafanya
wafugaji nchini kuacha ufugaji wa kuhamahama na kuingia kwenye ufugaji
wa kisasa ambao unatumia mifugo michache inayotokana na mbegu bora na
kupata mazao mengi ambayo yatawainua kiuchumi tofauti na ilivyo sasa
“Tunazo
aina tisa za mbegu kwa sasa ambapo kwa ngombe wa maziwa tuna aina ya
Frishan, Ashaya na Jezze, nyama na maziwa tuna ng’ombe aina ya Flegvi,
Simento na Saiwan na nyama tu.
"Tuna aina ya Borani na Bonsmara
na kazi yetu kubwa ni kuzalisha hizi mbegu na kuzisambaza kupitia
wahimilishaji kulingana na mhitaji nchini, ” amesema
Amefafanua
katika kuhakikisha elimu ya ufugaji kwa kutumia mbegu bora zinawafikia
wafugaji wengi kituo hicho kinaendelea kutoa elimu katika kanda zote
yanapofanyika maonesho ya Nanenane, hivyo wafugaji wanapaswa kutumia
fursa hiyo ili weweze kufuga kisasa
Kwa upande wake mmoja wa
wanufaika wa mbegu bora ya uhimirishaji Emmanuel Nanyaro ambaye ni
mfugaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Arusha amesema kwa sasa
anapata faida kubwa baada ya kupata ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa
hadi lita 40
Amesema baada ya kupata faida hiyo sasa ameamua
kujitolea kutoa elimu kwa wafugaji wengine ili kusaidia wafugaji
kutambua umuhimu wa kutumia mbegu bora zinazopatikana katika kituo cha
uhimilishaji NAIC ili waweze kujiinua kiuchumi.
“Nawashauri watu
wanaotaka kuingia kwenye ufugaji waje tupeane elimu ili waweze kuwa na
ng’ombe bora maana ukitaka kufuga lazima uwe na ng’ombe bora ambao
utapata mbegu kutoka kituo cha NAIC kilichopo hapa Arusha, ” amesema.



No comments:
Post a Comment