WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amekutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ajili ya kujitambulisha na kufanya naye mazungumzo.
Profesa Mkumbo
amekwenda kujitambulisha ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo kwenye
baraza la mawaziri na kuunda Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na kisha
kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa waziri wake na Dkt. Tausi Kida kuwa
Katibu Mkuu.
Pamoja na kukutana na Rais Mwinyi, Prof. Mkumbo pia
amekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa
Zanzibar Mudrik Soraga, ambapo katika mazungumzo yao, kwa pamoja
wamesisiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kwatika
kukuza uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.
Pro.
Mkumbo pamoja na ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea eneo la
uwekezaji wa bandari kubwa inayojengwa Zanzibar eneo la Mangapwani.
Ujumbe
ulioongozana na Waziri Prof.Kitila ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Mipango na Uwekezaji Dk.Tausi Kida, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu,
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu EPZA
Charles Itembe, Mkurugenzi Mkuu TIC Gilead Teri, Mkurugenzi wa
Miundombinu wa Mamlaka ya Bandari Dkt.Hussein Lufunyo Wakurugenzi wa
Wizara.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)



No comments:
Post a Comment