JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SERIKALI YAZIJIA JUU TAASISI ZA KIDINI ZINAZOFUNDISHA MAADILI YASIYO MEMA

Share This
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI yawajia juu viongozi wa Mashirikisho na Mabaraza ya kidini wanaofundisa maadili yasiyo ya kitanzania, wasio wasilisha taarifa mbalimbali za kila mwaka kama walivyoelekezwa katika sheria na kulipa ada kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun wakati akizungumza na viongozi hao katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Julai 04, 2023. Amesema kuwa wazingatie masharti ya usajili na sheria nyingine za nchi katika shughuli za Jumuiya wanazoongoza.

Mhandisi Masauni amesema kwa sasa taasisi nyingi za kidini zinaanzishwa pasipo kufuata sheria ya jumuiya ya sura 337 inayotaka kila kikundi au Jumuiya kusajiliwa ili iweze kufanya shughuli zake.

"Sote ni Mashuhuda kuwa zipo taasisi nyingi katika jamii yetu ambazo zinajiendesha pasipo kusajiliwa na hata uendeshwaji wake ni wa kutia mashaka." Ameeleza

Licha ya hayo ametoa wito kwa viongozi wa jumuiya za kidini nchini kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kusajili jumuiya na vikundi pale wanapoona uendeshaji wake unatia shaka au mafundisho yake si ya kimaadili ili kuiweka jamii katika hali ya usalama na amani.

Akizungumzia kuhusiana na migogoro inayozikumba jumuiya za kidini amewaasa kupitia katiba zao na kujiridhisha kama zinakidhi haja kwa wakati uliopo kwani itasaidia kuepusha migogoro isiyokuwa na sababu.

Akizungumza kuhusiana na Viongozi wa dini kufundusha bila kufuata maadili ya kitanzania Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na uzima, Antoni Lusekelo amesema kuwa viongozi hao endapo wakipatikana na hatia ya kufundisha mafundisho yasiyo na maadili wachukuliwe hatua na kupewa adhabu kali ili iwe funzo kwa viongozi wengine.

Kwa Upande wa Kaimu Shekhe Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Walid Kawambwa amesema kuwa mafunzo hayo yanatija kwa jamii kwani wataenda kutoa mafunzo wanayopewa kwa njia rahisi wakichanganya na maandiko ya Mwenyezi Mungu kila siku za ibada kulingana na kila taasisi siku wanayoabudu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun wakati akizungumza wakati wa kufungua kikao cha viongozi wa Mashirikisho na Mabaraza ya kidini katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Julai 04, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao cha viongozi wa Mashirikisho na Mabaraza ya kidini katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Julai 04, 2023.


Baadhi ya Viongozi wa dini wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 04, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad