JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RC PWANI ATOA RAI KWA HALMASHAURI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI ILI KUVUTIA WAWEKEZAJI

Share This

Mkurugezi  wa Halmashauri ya Kibaha Mji Mhandisi Mshamu Ali Munde  akifafanua jambo kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha, kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka 2021-2022.
Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Kihaha Mji, Musa Ndomba akifafanua jambo

Baadhi ya washiriki.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amezitaka Halmashauri kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ikiwa ni pamoja kupunguza migogoro ya ardhi.

RC Kunenge amesema hayo kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha, kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka 2021-2022 Kunenge amesema kuwa uwekezaji ndiyo kipaumbele cha Mkoa.

Amesema kuwa kutokana na Pwani kujipambanua kuwa ni Mkoa wa Viwanda ila changamoto ya migogoro ya ardhi bado ni tatizo sugu

"Haipendezi kuona mwekezaji anaweka uwekezaji lakini baada ya muda anaingia kwenye mgogoro wa ardhi hii itasababisha kasi ya uwekezaji kupungua,"amesema Kunenge.

Aidha amesema kuwa Mkoa una viwanda 1,522 ambapo vikubwa viko 27 na Halmashauri zinapaswa kuweka maandalizi mazuri ya uwekezaji pia kuanzisha vyanzo vipya vya uwekezaji.

"Kikubwa mnachopaswa kukifanya ni kupambana na migogoro ya ardhi ambayo kwa Mkoa ni mingi na haipaswi kuwepo kwani mwekezaji asingependa kuona migogoro ya ardhi ," amesema Kunenge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Musa Ndomba ameiomba serikali kuangalia maslahi ya Madiwani ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Ndomba amesema kuwa Mabaraza ya Madiwani yanashindwa kuzisimamia vizuri Halmashauri kutokana na maslahi yao kuwa duni lakini endapo maslahi yao yangekuwa mazuri wangeongeza ari ya usimamizi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa wanaendelea kuzifanyia kazi hoja za CAG ambapo nyingine tayari wameshazifunga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad