Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, ametembelea banda namba 13 la ushirikiano
baina ya NSSF na PSSSF kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Mfuko katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Balozi Siwa alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na
NSSF na PSSSF.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, amempongeza na kumkabidhi Joyce Sungura,
kadi ya uanachama wa NSSF baada ya kujiunga wakati alipotembelea banda
la NSSF katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
NSSF inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi
ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima,
wavuvu, wafugaji, wachimba wadogo wa madini, mama lishe, bodaboda na
wajasiriamali wengine wote ambao wanapofika katika banda hilo wanapewa
elimu na kuandikishwa kuwa wanachama wachangiaji.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, amekutana na Kamishna wa Polisi, Utawala
Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Suzan Kaganda pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji Wakala Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar, Juma Burhan
Mohamed, alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere, nakujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko katika
maonesho hayo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Fatma
Hamad Rajabu, ametembelea banda namba 13 la ushirikiano baina ya NSSF na
PSSSF kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment