JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Mtandao wa Bolt unaongoza kwa usafirishaji Ulaya umeongeza wateja milioni 150 na kuteua CFO mpya

Share This

● Ilianzishwa nchini Estonia mwaka wa 2013, Bolt sasa inafanya kazi katika zaidi ya nchi 45 na miji 500.

● Mikko Salovaara ametajwa kuwa CFO mpya, Bolt inatarajia kupata faida kamili katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

● Taarifa inakuja huku biashara ikitimiza miaka kumi tangu ilipoanzishwa na Markus Villig aliyekuwa na umri wa miaka 19 wakati huo.

Kampuni ya Bolt inayoongoza kwa huduma ya usafiri mtandaoni Ulaya imetangaza kuwa imeongeza wateja milioni 150 katika zaidi ya nchi 45 na miji 500.

Wateja milioni 150 wa Bolt wametawanyika katika kundi lake la bidhaa za usafiri ambao ni pamoja na huduma ya taxi mtandao, kukodisha pikipiki, utoaji wa chakula, uwasilishaji wa mboga mboga, Bolt Drive, huduma ya kukodi magari ya kuendeshwa na mteja, Bolt Business na huduma ya uhamaji ya mashirika. Bolt pia imetangaza  kuna zaidi ya washirika milioni 3.5 (madereva na wasafirishaji) wanaotumia programu hiyo kujipatia riziki, wakiwemo zaidi ya milioni 1 barani Afrika pekee.

Takwimu mpya zimetolewa siku ambayo Mikko Salovaara ametangazwa kuwa Afisa Mkuu mpya wa Fedha wa Bolt (CFO) siku chache baada ya Ripoti ya mwaka 2022 ya biashara inaonyesha kuwa imepata faida kubwa ya kila mwaka.

Licha ya hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwepo ikiwa pamoja na kuongezeka kwa mfumuko wa bei, kupanda kwa viwango vya riba na mtazamo usio na uhakika wa uchumi  katika masoko mengi, Bolt iliongeza mapato yake kwa kiasi kikubwa na iko mbioni kuwa jukwaa la kwanza la usafirishaji  Ulaya kupata faida kamili ndani ya miezi 12 ijayo.

Markus Villig, Mwanzilishi na Mkurugenzi  Mtendaji wa Bolt, alisema: "Kanuni zetu za msingi zimesalia zile zile tangu tulipoanzishwa miaka kumi iliyopita - kwa kuwa jukwaa la usafirishaji lenye ufanisi zaidi duniani tunaweza kutoa thamani kubwa kwa wateja na washirika wetu. Kuwa na huduma bora na bei zinazovutia huchangia ukuaji wa sekta yetu, na tunajivunia sasa kuhudumia wateja milioni 150 katika nchi 45. Kiwango hiki kikubwa kitasababisha kupata faida katika kipindi cha miezi 12 ijayo.”

"Kuleta utaalam wa Mikko kwenye wakati huu muhimu kwa biashara itakuwa muhimu sana tunapoendelea kuzingatia ukuaji wa muda mrefu na endelevu, na kuanza maandalizi yetu ya IPO."

Mikko Salovaara, Afisa Mkuu wa Fedha wa Bolt anayekuja, alisema: "Katika tasnia ambayo inaonekana kuwa ngumu kufanya kazi kwa faida, Bolt inasimama imara juu ya washindani wake. Utamaduni wa kuongeza ufanisi wa uendeshaji ambao uliwekwa na Markus miaka kumi iliyopita unaendelea kuongoza biashara leo na umeiacha Bolt ikiwa katika nafasi nzuri ya kufikia na kudumisha faida ya muda mrefu. Ninatazamia sehemu ya hatua hii inayofuata ya biashara katika safari ya Bolt wakati  inapojiandaa kuelekea kwenye IPO, Mikko atachukua jukumu lake jipya  baadaye mwezi huu.

Ongezeko jipya la wateja milioni 150 na uteuzi wa Mikko Salovaara kama CFO imetangazwa kama alama ya Bolt miaka kumi tangu kuanzishwa kwa biashara hiyo na Markus Villig mwenye umri wa miaka 19 wakati huo huko Tallinn, Estonia.

Baada ya kuanza kama programu ya kukaribisha wapanda taxi mtandao mnamo 2013 wakati Markus aliajiri madereva binafsi kwenye mitaa ya Tallinn, Bolt imekuwa na ukuaji mkubwa katika miaka ya hivi karibuni. Ilizindua utoaji wa huduma ya chakula mnamo 2019, ikifuatiwa na kukodisha pikipiki mnamo 2020, na huduma ya usafirishaji wa mboga mboga na huduma ya kutumia magari  mnamo 2021.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad