Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KAMPUNI
DPO Pay inayoongoza kwa huduma za malipo ya kidijitali imetambuliwa na
kupewa kibali na Benki Kuu ya Tanzania (BoT )kutoa huduma za malipo
nchini.
Kwa mujibu wa DPO Pay yenye makao makuu yake nchini
Kenya, ni kwamba itaendeleza shughuli zake nchini baada ya kuwa
imetambuliwa kwa mujibu wa sheria na kupata leseni.
Akizungumza
leo jijini Da es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa DPO Pay, Bi Janeth Upendo
Kwilasa amesema wanafurahi kupokea leseni hiyo kutoka Benki Kuu ya
Tanzania ( BoT).
Amesema kwa kuzingatia dhamira yao thabiti ya
kuongeza wigo wa utoaji huduma zao katika nchi za Afrika Mashariki,
kibali hicho ni sehemu ya kuonesha nia yao na uthabiti wao wa kufuata
taratibu zote za kisheria na kiutaratibu katika kuendesha shughuli zao
nchini Tanzania.
Akieleza zaidi amesema DPO Pay ambayo sasa ipo
chini ya shirika la Network International, shirika ambalo ni mwezeshaji
mkuu wa biashara za kidigitali katika eneo la Afrika Mashariki na Kati
iko tayari kutoa huduma zake nchini Tanzania.
Janeth
amebainisha utayari wa DPO Pay katika kuchagiza na kuwezesha
ujumuishaji kifedha kwa makundi mbalimbali na ustawi wa biashara
kidigitali.
Amesema mifumo ya DPO ni thabiti na inawahakikishia
watumiaji wake kama wafanyabiashara kufanya miamala kwa urahisi,
ufanisi, uhakika na haraka zaidi huku ikihawakikishia watumiaji wake
ulinzi wa taarifa zao.
“DPO Pay ina mifumo thabiti
inayohakikisha ulinzi wa taarifa za mtumiaji na ubora wa huduma. Kwa
kutumia DPO Pay Mobile inayopatikana (istore/playstore), wateja wetu
wanauhakika wakupata huduma mbalimbal katika ubora na upekee,”
amesisitiza Janeth.
Aidha amesema DPO Pay tayari inafanya kazi
Zanzibar na kutumiwa na wafanyabiashara wa hoteli, usafiri na watu
binafsi kuupokea na kufanya malipo kupitia DPO Pay.Huduma za DPO Pay
zinatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara, na watu binafsi kuendesha
malipo kidigitali ndani na nje ya nchi.
"Kwa sasa DPO Pay
inaendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika. Pia kupitia DPO
Pay, mteja anaweza kufanya malipo kupitia kadi ya benki, simu, kuhamisha
fedha.",ameeeleza Janeth.
No comments:
Post a Comment