Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Josephat Lotto na Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa wakikata utepe kuzindua mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof.Josephat Lotto na Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa wakisaini mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
KATIKA kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wamesaini Mkataba wa makubaliano leo Julai 14,2023 jijini Dar es Salaam. Ili kutekeleza mradi huo zimetengwa dola milioni 10.5.
Na katika pesa hizo zimetengwa fedha shilingi milioni 257 kwaajili ya kuboresha mashirikiano kati ya IFM na NEEC.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Josephat Lotto, ameseama kuwa makubaliano hayo yatasaidia kuwa na ushirikiano wa moja kwa moja na Vyuo vya elimu ya juu na taasisi zinazo saidia wananchi.
Taasisi za umma na taasisi binafasi na vyuo kwaajili ya mashirikiano ambayo yatawawezesha wanafunzi kwenda kwenye mashirika, kampuni, Viwanda kwenda kupata uzoefu wa yale wanayofundishwa ili wakihitimu wachangie moja kwa moja kwenye uchumi wa nchi.
Amesema kuwa utiaji saini makubaliano hayo unaonesha dhahili mshikamano
Kabla ya Mradi huu ilibainika kwamba kile taasisi za elimu wanachotoa ni kunatofauti kubwa na kile kinachohitajika sokoni.
Amesema mradi huo utawawezesha wahitimu kuuzika kwenye soko lakini pia kuchangia kwenye ufanyaji kazi zenye matokeo mazuri katika uchumi wa nchi.
Amesema wahitimu wanaweza kuwa na taaluma lakini hawana ujuzi wa kutosha wa kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii pia kutokuajirikaa na kutokuweza kuajiri wengine.
Lengo la makubaliano hayo ni kuhakikisha wanaboresha mitaala, kuboresha Managementi ya elimu.
Kwa Upande wa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa amesema kuwa Makubaliano yaliyoyafanya leo yanatija kubwa hasa kwenye masuala ya kifedha na kila mtu lazima awe na ujuzi wa kutafuta fedha na kuzitawala.
"Ujuzi wa Fedha haupo sana katika jamii ya watanzania ndio maana watu wengi wanapata mikopo, wanapata matatizo ya kifedha kwa sababu ya kukosa nidhamu ya fedha." Ameeleza.
Akielezea kuhusiana na faida za makubaliano hayo, Beng'i amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia hasa watanzania ambao hawajaenda shule nao wanaweza kupata fursa ya kupata ujuzi zaidi kupitia mashirikiano kati ya NEEM na IFM.
Amesema pia kunavijana wanaopata elimu IFM na baadae wanaweza kuajiriwa au kuingia kwenye biashara hao pia watanufaika na makubaliano hayo mbayo yamefanyika leo.
"Na hapo tunaona itatusaidia kuwapa Mrejesho chuo, mambo gani ambayo yanaweza kuingia kwenye mitaala yao, mambo gani ambayo wanaweza kuyafanya katika kutoa vijana bora katika Uchumi wa kisheria." Amesema
Amesema changamoto kubwa iliyopo hapa nchini ni kutokuwa na elimu ya fedha isipokuwa wanaosoma IFM ndio wana elimu ya fedha, lakini ....."Ifahamike kuwa mwanadamu anapozaliwa hapa duniani katika vitu mhimu ambavyo lazima avifanye ni kula chakula na kushika fedha mwa kufundishwa au hukufundishwa lazima utashika fedha, uwe umesoma au hujasoma utashika fedha." Amesema Beng'i
Amesema kuwa elimu na nidhamu inahitajika kuituza fedha, ingawa watu wengi hawana elimu hiyo na jinsi ya kuitunza na kuiwekea bajeti fedha.
Aidha mkataba huo wa ushirikiano utasaidia ukuaji wa elimu ya fedha hapa nchini na kuendeleza mpango mkakati wa fedha ambao serikali imeutengeneza ikiwa watekelezaji wa huo mpango ni wananchi kwa ujumla.
Beng'i amesema Watanzania wajihusishe zaidi kufahamu mambo ya fedha lakini wajihusishe na mifumo rasmi ya fedha, hasa benki, na michakato ya kiteknolojia ambapo itawasaidia watanzania wote wajumuike katika huduma za kifedha.
Akizungumzia kugusiana na uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na kwamba uwezeshaji ni pesa au mitaji lakini ni pamoja na ujuzi ambo ni mhimu katika kuhakikisha kwamba kila mmoja anapewa fursa.
Mwanasheria wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, wakisaini mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof Josephat Lotto na Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa wakibadilioshana mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Josephat Lotto akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issaakizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Mfanyakazi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dkt.Grace Kazoba akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano leo Julai 14, 2023 kwaajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Picha za pamoja.
No comments:
Post a Comment