Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mwakiselu Mwambange akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 7, 2022 kwenye Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanavyoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba.
Mmoja ya wafanyakazi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda lao lililopo katika jengo la Wizara ya fedha jijini Dar es Salaam leo Julai 07, 2023.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KATIKA kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) wameaokoa kiasi cha shilingi bilioni 130 katika vifaa na huduma mtambuka.
Kwenye manunuzi ya magari ya serikali GPSA imeokoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 36 ambazo zimetokana na wazabuni kuwapatia punguzo kutokana na kununua magari mengi hivyo kuzishauri taasisi zingine kuigia mfumo wao wa kujadiliana ili kupata punguzo la manunuzi.
Na katika kipindi cha Miaka mitano, imesema imeweza kuokoa kiasi cha bilioni 21 kutokana na Ugomboaji, uondoshaji wa mizigo ya serikali mipaka, bandarini pamoja na viwanja vya ndege.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa GPSA, Mwakiselu Mwambange, jijini Dar es Salaam leo Julai 7, 2022 kwenye Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanavyoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba. Amesema fedha hizo zimeokolewa kuanzi mwaka 2018 hadi 2023.
Pia kwa upande wa ununuzi wa vifaa mbalimbali amesema kuwa GPSA inasaidia serikali kupata vifaa mbalimbali bila kupitia katika mchakato wa zabuni kwa sababu Wakala hiyo inakuwa imeshafanya michakato yote ya awali.
"Katika kipindi hiki tumehakikisha taasisi imekwenda kufanya shughuli zake kwa kutumia mifumo ya tehama ili kurahisisha utendaji kazi na kwa ufanisi." Amesema
Mwambange amesema kuwa Selikali imeanzisha mfumo jumuishi wa GIMIS ambao umejumuisha majukumu ya GPSA ambapo unamrahisishia kazi, mteja anayehitaji mafuta pamoja na vifaa mtambuka katika Wakala huo.
Amesema katika Mfumo huo wa GIMIS umeweza kuwaunganisha wadau wote ambao wapo katika vituo vya ununuzi wa magari Serikalini ambao ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ujenzi pamoja na Wizara ya Fedha.. Kupitia Mfumo huo wa GIMIS taasisi ya Serikali inapotaka kununua magari hailazimiki kwenda ofisi ya waziri mkuu moja kwa moja au kuandika barua, kupitia mfumo anawasilisha maombi, yanatoka kwenye mfumo yanaenda wizara ya ujenzi ya natufikia GPSA na sisi tunaendelea na ununuzi wa magari, mteja tumemrahisishia anaonana na sisi pale anapokuja kukabidhiwa gari tuu.".... Ameeleza Mwambange
Amesema utaratibu wa sasa hivi ni mzuri na nirahisi tofauti na siku za nyuma ambapo ilitakuwa mteja kundika barua na kufata taratibu, mfumo huo unarahisisha kupata taarifa na kujua ombi lake lipo Sehemu gani pia inarahisisha kupata huduma.
Amesema kuwa pamoja na kuwa na mfumo huo lakini wanamatarajio ya kuanza kutoa huduma ya mafuta kwa kutumia E-card ( kadi za kieletroniki) ambazo zitawasaidia wateja kupata huduma ya mafuta bila mwingiliano wowote watoa huduma pamoja na kupata mafuta wakati wote.
Mwambange ametaja vituo vya mafuta kuwa ni Dar es Salaam- kurasini na Kinondoni, Dodoma- mji wa Kiserikali Mtumba, Simiyu ambako wanamalizia maboresho pamoja na Njombe.
Aidha akizungumzia kuhusu Maonesho ya sabasaba ya mwaka huu 2023 amewakaribisha wananchi kujitokeza kwenye banda lao lililoko kwenye banda la wizara ya fedha ili kuweza kupewa taarifa mbalimbali wanazotoa.
Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi walio tembelea banda lao leo Julai 07, 2023 kwenye maonesho ya biashara ya 47 yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment