JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WALIOVAMIA HIFADHI YA CHEMCHEM MAJI MOTO RUFIJI WAMEGEWA ENEO KWENYE HIFADHI

Share This

 




Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
WANANCHI  waliovamia Eneo la Hifadhi la Chemchem ya Maji ya Moto Rufiji- wamegewa Eneo kwenye hifadhi hiyo.


Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge wakati akitoa tamko la kuhitimisha Mgogoro huo ikiwa ni Utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Mawaziri iliyotokana na Kamati ya Mawaziri wa nane wa Kisekta walioshughulikoa migogoro hiyo.

Akitoa maagizo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Major Edward Gowele Mkuu wa Wilaya ya Rufiji- amewataka Wananchi wanaozunguka maeneo hayo kutovamia eneo hilo na kuagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS na Kamshna Msaidizi wa Ardhi kupima upya eneo hilo la Hifadhi na kuandaa GN Mpya.

Aliwataka TFS kuchonga Barabara kuzunguka eneo hilo ili Kuweka Kinga kati ya Wananchi na Hifadhi.

Katika Hatua Nyingine alitembelea Delta ya Mto Rufiji- na kuhitimisha Mgogoro wa Ardhi uliopo la Wananchi kuendesha shughuli za kibinadamu katika hifadhi hiyo ya Misitu ya Mikoko na mazalia ya Samaki .

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa kwenye Kuhitimisha Mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Col Samwel Kolombo alipiga marufuku ukataji wa Misitu ya Mikoko ovyo.

Aidha alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kibiti kutoa Elimu ya uhifadhi wa Wananchi na kuwawezesha vifaa vya kuvulia samaki kwenye Maji marefu.

Alisisitiza pia kuanzisha kwa vikundi vya uhifadhi BMU ili kuimariasha ulinzi wa hifadhi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad