JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SERIKALI KUJENGA NYUMBA 212 ZA WATUMISHI WA KADA ZA ELIMU NA AFYA KUPITIA MRADI WA SEQUIP

Share This

 


Na James Mwanamyoto – OR-TAMISEMI
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali kupitia mradi wa SEQUIP imekamilisha mchakato wa kujenga nyumba 212 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi wa kada za elimu na afya nchini.

Mhe. Ndejembi amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Shally Josepha Raymond aliyetaka kujua jitihada zilizofanywa na Serikali katika kutatua changamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi wa kada za elimu na afya.

Mhe. Ndejembi amesema, Serikali inaendelea na jitihada za kukabiliana na upungufu wa nyumba za watumishi wa kada za elimu na afya hususani waliopo vijijini.

“Ni kweli kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za watumishi waliopo vijijini hususani wa kada ya elimu na afya, hadi Mei 2023 idadi ya nyumba za walimu zilizopo vijijini ni 55,097 wakati upungufu ni nyumba 255,097 na idadi ya nyumba za watumishi wa kada za afya zilizopo vijijini ni 7,818 na upungufu ni 15,272,” Mhe. Ndejembi amefafanua.

Mhe. Ndejembi amesisitiza kuwa, ni wajibu wa halmashauri kuanza kutenga fedha katika mapato yao ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa kada ya elimu na afya ili kuunga mkono jitihada za Serikali kuu kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshapeleka fedha vyingi kwa ajili ya ujenzi wa maboma, madarasa, zahanati na vituo vya afya katika halmashauri zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad