JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MWANAFUNZI ALIYEPOTEA MBEYA APATIKANA, APIMWA HANA MIMBA

Share This

 


Na  Avila Kakingo, Michuzi TV
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumpata mwanafunzi wa kidato cha tano mchepuo wa PCB katika Shule ya Sekondari Pandahili, Ester Noah Mwanyilu [18] Mkazi wa Forest Jijini Mbeya aliyekuwa amepotea tangu Mei 18, 2023.

Kwa Mujibu wa tarifa iliyolewa leo Juni 23, 2023 na Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzuga imesema kuwa Mwanafunzi huyo amepatikana Juni 23, 2023 majira ya saa 05:30 asubuhi huko maeneo ya Ifisi katika Mji Mdogo wa Mbalizi baada ya timu ya makachero ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufuatilia taarifa mbalimbali zilifanikisha kumpata mwanafunzi huyo akiwa katika chumba cha kupanga cha mwanamke aitwaye Azurat Abdul Mohamed [24] Mfanyabiashara wa Genge na Mkazi wa Ifisi – Mbalizi.

“Kwa mujibu wa maelezo ya Azurat Abdul ni kuwa binti huyo aliletwa kwake na kijana mmoja anayemfahamu kwa jina la Baba Jose ambaye ni mteja wake wa kumletea Mkaa kwa Magunia hapo Gengeni kwake. Alipomleta takribani wiki mbili zilizopita alimueleza kuwa huyo ni mke wake ametoka mkoani Morogoro hivyo anamuomba ampe hifadhi wakati yeye akitafuta chumba cha kupanga na mara atakapopata chumba atakwenda kumchukua. Binti huyo Alijitambulisha kwa Azurat Abdul kwa jina moja la Erica na kwamba anatokea Morogoro.” Imeeleza

Awali Mei 18, 2023 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipata taarifa za kupotea kwa mwanafunzi huyo na kuanza uchunguzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwahoji viongozi wa Shule hiyo, wanafunzi wenzake, majirani na wale wote waliokuwa wametajwa akiwaomba msamaha kwa maamuzi aliyoyachukua kupitia ujumbe wa maandishi aliouacha mwanafunzi huyo kabla ya kutoweka shuleni hapo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hili ikiwa ni pamoja na msako wa kumtafuta mtuhumiwa aliyekuwa akiishi naye.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad