JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA KILO 38.84 ZA BANGI

Share This

 

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kibaha, imemuhukumu Abubakar Rajabu Mbaje kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 38.84 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Hukumu katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka 2022 imesomwa Mei 31, 2023 na Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Mshtakiwa Mbanje alikamatwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Mei 19, 2022 huko katika eneo la bandari bubu iliyopo Mlingotini - mji mpya wilaya ya Bagamoyo akiwa na Kilo 38.84 za Dawa ya Kulevya aina ya Bangi alizokuwa akizisafirisha kwa kutumia pikipiki.

Baada ya kukamatwa mshtakiwa alifikishwa mahakama na kusomewa shtaka lake la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Wakati wa usikilizwaji kwa kesi hiyo, upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na mawakili wa serikali wawili, Rachel Morgan na Gloria Simpassa ambapo jumla ya Mashahidi 6 wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi wao ambao uliweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa alisafirisha dawa za kulevya.

Mshtakiwa katika kesi hiyo aliwakilishwa na Wakili Idd Msawange ambapo walikuwa na mashahidi wanne akiweno mshtakiwa mwenyewe.

Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani aliiomba Mahakama imuonee huruma na kumuachia huru.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Salumu amesema mahakama imetoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa kwa mujibu wa sheria na pia ili iwe fundisho kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Pia pamoja na adhabu hiyo, mahakama imeamuru pikipiki aliyotumia mshtakiwa kutenda kosa la kusafirisha dawa hizo za kulevya aina ya bangi itaifishwe na kielelezo ambacho ni dawa za kulevya aina ya Bangi kiteketezwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad