JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DIWANI KATA YA SANDALI MH. KABALIKA AGAWA VIAKISI MWANGA KWA BODABODA ZAIDI YA 150

Share This

Diwani wa Kata ya Sandali Mh. Christopher Kabalika Mwasansu 'Kabalika'  mwenye suti nyeusi katikati akizungumza mara baada ya kukabidhi viakisi mwanga (reflector) zaidi ya 150 kwa vijana waendesha bodaboda katika ya kata ya Sandali iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Mei 28, 2023.
Diwani wa Kata ya Sandali Mh. Christopher Kabalika Mwasansu 'Kabalika' akiwa katika picha ya pamoja na waendeha pikipiki maarufu kama bodaboda Mei 28, 2023 jijini Dar es Salaam mara baada ya  kugawa viakisi mwanga (reflector) zaidi ya 150.
Diwani wa Kata ya Sandali Mh. Christopher Kabalika Mwasansu 'Kabalika' akiwakabidhi viakisi mwanga (reflector) zaidi ya 150 kwa vijana waendesha bodaboda katika ya kata ya Sandali iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Mei 28, 2023.


DIWANI wa Kata ya Sandali Mh. Christopher Kabalika Mwasansu 'Kabalika' amegawa viakisi mwanga (reflector) zaidi ya 150 kwa vijana waendesha bodaboda katika ya kata ya Sandali iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine Mh. Kabalika amesisitiza bodaboda wote kufuata sheria zilizopo na kuwa walinzi wa jamii kwani kazi yao ya usafirishaji kwa njia ya pikipiki ni muhimu sana na inahudumia kundi kubwa la wananchi.

Akizungumza mara baada ya kukbidhi Viakisi Mwanga hivyo jijini Dar es Salaam  Mei 28, 2023. Amesisitiza kwa vikundi vyote vya bodaboda kuvaa viakisi mwanga zitakazowatambulisha vituo vyao na eneo waliopo na kuondoa hofu kwa abiria wao.

Mh Kabalika amesema huu ni mwanzo tu kwa kundi hili la bodaboda kwani anaandaa kikao kazi cha kuwasikiliza na kujua shida na kero zinazowakabiri bodaboda ili azipatie ufumbuzi.

"Kundi hili ni kubwa kama tutajipanga vizuri tunaweza kufanya jambo kubwa mfano kuandaa SACCOS ya bodaboda yenye kuweza kuwasaidia hata kupata urahisi wa pikipiki.

Ndugu zangu ukitaka kufika haraka nenda mwenyewe lakini ukitaka kufika mbali nenda na wenzako". Ameeleza Mh. Kabalika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad