
Meridianbet kama ilivyo desturi na utamaduni wao wamekuwa wakijitahidi kushirikiana na jamii na kusaidia makundi yenye uhitaji na yanayokumbwa na changamoto mbalimbali.
Jana Meridianbet waliwatembelea waathirika wa madawa ya kulevya
wanaopambana kuachana na matumizi ya madawa hayo chini ya taasisi ya Pillimissana
Foundation huko Kigamboni.
Taasisi hiyo imeanzishwa
takribani miaka kumi iliyopita, ikijishughulisha na watu wenye uraibu wa wa
madawa ya kulevya, na kuwasaidia kupambana na hali hiyo.
Timu ya Meridianbet ilifika Sober House ya Pillimissana Foundation, Kigamboni
na kupata mapokezi mazuri chini ya msimamizi wa kituo, ambaye alitoa ufafanuzi
wa mambo mbalimbali, ikiwemo takwimu za wa waraibu waliofanikiwa kuhudumiwa
ndani ya kituo hicho, pamoja na changamoto wanazo pambana nazo pale wanaporudi
kwenye jamii.
Pia alieleza kituo hicho
kimefanikiwa kutoa huduma kwa zaidi ya waraibu elfu mbili tangu kuanzishwa kwa
kituo hicho mwaka 2012.
Timu ya Meridianbet ikiongozwa na Afisa Masoko wa taasisi hiyo Bwana
Twaha Ibrahim, na balozi wa Kampuni hiyo bwana Jacob Mbuya walibainisha kuwa ni
utaratibu wa Meridianbet kurejesha kwa Jamii, na wakati huu wameona wanaguswa
na jitihada za Pillimissana Foundation na kuwaunga mkono katika jitihada hizo.
Timu ya Meridianbet iliunga mkono jitihada za Pillimissana Foundation
kwa kutoa baadhi ya mahitaji ya msingi kama mchele, sukari, unga wa sembe na ngano,
mafuta ya kupikia pamoja na Sabuni.
Meridianbet baada ya kukabidhi vitu hivyo kwa msimamizi wa
kituo walipata wasaa wa kuonana na waraibu na kuzungumza nao maneno machache
kuwatia moyo na kuwapongeza kwa kukubali kupata tiba ili kurejea katika hali
zao za kawaida na kuongeza nguvu kazi ya taifa..
Pia mmoja wa waraibu, ambaye
tumemhifadhi jina lake alipata nafasi ya kuzungumza na kuwawakilisha wenzake na
kuishukuru sana timu ya Meridianbet kwa moyo waliouonesha na kuwataka wasiache
kuendelea kurejesha kwa Jamii, kwani jambo zuri na la kuigwa.
Timu ya Meridianbet, inampongeza
mratibu wa kituo hicho kwenye taasisi ya Pillimissana Foundation, Pilli Ramadhani Missana. Ujumbe kutoka kituo hiki ni kuwa jamii inapaswa
kutowatenga waraibu pale wanaporudi mitaani kwani inawavunja moyo na inaweza kuwa
sababu ya kurejea kwenye utumizi wa madawa ya kulevya.
Meridianbet ambao ni mabingwa na wakongwe wa michezo ya
kubahatisha kupitia tovuti na kasino ya mtandaoni, wakiwa na Jackpot kibao kupitia Meridianbet Casino, wamesisitiza kupitia afisa masoko wao Mr.
Mohammed kuwa wataendelea kuwa karibu na jamii na kuwashika mkono wenye
uhitaji.


No comments:
Post a Comment