Mmoja ya jopo la majaji walio pitia kazi 598 za waandishi wa habari akizungumzia changamoto walizozipata wakati wa kupitia kazi za waandishi wa habari na kupata kazi 60 zilizo bora zaidi kwaajili ya kuwatunukia tuzo waandishi wa kazi hizo kwa mwaka 2021. kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya MaaNdalizi EJAT, 2021, Kajubi Mukajanga.
Na Avila Kakingo, Michuzi TV.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika utoaji Tuzo za umahiri wa uandishi wa habari
Tanzania (EJAT), 2021 na ndiye atakaye mkabidhi Tuzo mshindi wa jumla
pamoja na mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa
Habari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Mei 19 2021 ,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi EJAT, 2021, Kajubi Mukajanga amesema
kuwa tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mei 28, 2022 katika ukumbi wa
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa idadi ya wateule wa EJAT 2021 kwa upande wa wanawake ni 28 ambayo
ni sawa na asilimia 47, ikiwa ni ongezeko la asilimia tatu ukilinganisha
tuzo zilizopita ambapo wanawake walikuwa ni 26 sawa na asilimia 44
walioingia kwenye hatua hiyo kwa mwaka jana. Na wateule wanaume ni 32
sawa na asilimia 53.
Amesema
kuwa jopo la Majaji lilikaa na kupitia kazi 598 za waandishi zilizokuwa
katika makundi 20 yanayoshindaniwa katika tuzo za umahili wa Uandishi
wa habari Tanzania (EJAT) 2021 na kufanikiwa kuteua waandishi 60 ambao
kazi zao zimeonekana kuwa bora zaidi.
Kati ya wateule hao 60 tisa wanaadikia Runinga, 12 vyombo vya Mtandaoni, wanne redio na 31 wanaandikia Magazeti.
Kati
ya wateule 28 wanawake 18 wanatoka katika magazeti, runinga wametoka
watatu, radio wawili na vyombo vya habari vya mtandaoni watano, Kwa
upande wa waandishi wa habari wanaume, magazeti wametoka 12, runinga
waandishi sita, radio wateule sita na vyombo vya habari vya mtandaoni
wateule saba." Amesema Mukajanga.
Amesema
Kwa mujibu wa majaji wa EJAT 2021, kazi za mwaka huu, zimeonyesha kuwa
na kiwango cha juu ukilinganisha na mwaka jana. Hiyo ni pamoja na
kiwango cha waandishi wa habari wa vyombo vya mtandaoni kuonyesha
kukomaa zaidi katika kazi zao na mwamko wa ushiriki katika Tuzo hizo.
Makundi
yanayoshindaniwa katika Tuzo za EJAT 2021 ni Tuzo ya Uandishi wa Habari
za Uchumi, Biashara na Fedha, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na
Utamaduni, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo,
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu, Tuzo ya Uandishi wa Habari za
Utalii na Uhifadhi, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Tuzo za
Uandishi wa Habari za Data, Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za
Binadamu, Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji.
Mpiga
Picha Bora- Magazeti, Mpiga Picha Bora- Runinga, Mchora Katuni
Bora,Tuzo ya uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto, Tuzo ya Uandishi wa
Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini, Tuzo za Uandishi wa Habari
za Walemavu, Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya na Tuzo ya Uandishi wa
Sayansi na Teknolojia.
Tuzo
hizo zimefadhiliwa na Wajibu Institute, Natural Resources Governance
Institute NRGI, washiriki, Kituo cha Msaada wa Kisheria, na Haki za
Binadamu (LHRC), Busota Inn, Serena hotel Dar es Salaam, Coca Cola,
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Azam Media, Twaweza na Tume ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH).
Hii itakuwa ni mara ya 13 kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi katika mwaka 2021.


No comments:
Post a Comment