Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kujengwa misingi bora ya uadilifu kwa viongozi wa ngazi mbali mbali ni umuhimu katika kuleta maendeleo na kuwepo amani ya kweli nchini.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema katika jimbo la Bubu wilaya ya Magharib ‘A’ aliopozungunza na Viongozi wa Chama hicho akiwa katika mfululizo wa ziara yake ya kichama tokea alipochaguliwa kushika wadhifa huo Januari 29 mwaka huu.
Mhe. Othman amesema kwamba uadilifu ndio njia muhimu inayojenga misingi bora ya kuleta haki ndani ya jamii na taifa kwa jumla, jambo pia linalochangia kuwepo na kuendeleza amani ya kweli na maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Aidha amesema kwamba kuwepo kwa misingi ya namna hiyo pia kunasaidia kuondosha na kudhibiti vitendo vya rushwa na ubadhirifu katika nchi, na hivyo wananchi wote kupata haki zao wanazostahiki kupitia sekta mbali mbali za huduma zinazotolewa kwa wananchi nchini.
Amesema katika taifa lolote lile duniani, hakuwezi kuwepo amani ya kweli bila ya kuwepo haki inayochungwa na kutolewa katika misingi bora iliyowekwa na kusimamiwa ipasavyo na viongozi wa ngazi zote sambamba na kuchukia na kukemea rushwa.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba Zanzibar inautajiri mkubwa na inafahamika kwamba ni pahala pazuri na pia kituo muhimu cha kiuchumi duniani, lakini kinachohitajika ni kuwepo uwajibikaji na uadilifu wa viongozi katika kusimamia shughuli mbali za nchi yao.
Hivyo Mhe. Othman amekumbusha haja ya jamii na taifa kwa jumla kuwa na mpango madhubuti wa kuwaandaa vijana kimaadili ili wawe na uwezo mkubwa wakushika dhamana na nafasi mbali za uongozi nchini.
Naye Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Salim Biman, amewakumbusha wanachama na viongozi wa chama hicho kuendeleza mashirikiano na kuhakikisha kwamba wanafuata taratibu za vikao katika kusimamia masuala mbali mbali ya chama hicho.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ismail Jussa, amewataka wanachama wa chama hicho kujitahidi kutoa kipaumbele na kujitolea katika kuendeleza kazi za chama kwa kuwa kufanya hivyo ndio kufuata nyayo za Marehemu maalim Seif Sharif Hamad aliyejitolea muda wake wote katika kuwatumika watu bila kuchoka.
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WANACHAMA WA ACT BUBUBU
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.


No comments:
Post a Comment