Adeladius Makwega-WUSM.
Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Paulne Gekul Machi 21. 2022 Jijini Dodoma amewapongeza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kwa kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa wanaweza kusimama mbele na kuwawakilisha wenzao katika mkutano huu wakitoka katika idara na vitengo vyao.
“Tunatambua kuwa kila mtumishi wa wizara hii anafanya kazi kwa juhudi kubwa na mambo mengi sana ambayo yanaonekana kwa macho, naomba nitumie fursa hii kuwapongezeni kwa juhudi zenu hizo.”
Naibu Waziri Gekul aliongeza kuwa yeye jukumu lake ni kumsaidia Waziri Mchengerwa kwa kuyafanikisha malengo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na taifa letu linasonga mbele.
Awali kabla Naibu Waziri Gekul kuzungumza katika Baraza hilo la Wafanyakazi, kwa pamoja wajumbe wote na waalikwa kwa bashasha walisimama, wakishikana mikono na waliuimba wimbo wa Mshikamano Daima (Solidarity Forever)
“Wafanyakazi wote tujiunge pamoja,Wafanyakazi wote tujiunge pamoja, wafanyakazi wote tujiunge pamoja. Kujitenga ni hatari. Haya shime tujiunge, haya shime tujiunge, haya shime tujiunge. Kujitenga ni hatari.”
Naibu Waziri Pauline Gekul aliipamba marufaa ya kusemea katika mkutano huo kwa kuvalia gauni maalumu ya kitenge cha rangi mchanganyiko na chenye maua rangi ya njano,kijani, kijivu na nyeusi3 ambapo iliagizwa katika mikutano yote ya Baraza la Wafanyakazi ijayo kutavaliwa mavazi ya vitenge.
GEKUL ANOGESHA MARUFAA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.


No comments:
Post a Comment