JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Airtel, benki ya Letshego Wakabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya mwisho ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba

Share This

 AIRTEL yashirikiana na benki ya Letshego kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya mwisho ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo kwa kushirikiana na benki ya Letshego wamekabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya mwisho ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba.

Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ni ya wiki sita, ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kujiwekea utaratibu wa kujiwekea Akiba.

Washindi hao ni Emmanuel Lugakingira mkazi wa Mikocheni Dar es Salaam ambaye amekabidhiwa milioni tano na Nigwike Kibona ambaye amekabidhiwa milioni moja.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza washindi hao kwa kushinda na pia kwa kujiwekea Akiba.

Kampeni hii ya Weka Akiba Ushinde na Airtel Timiza ilikuwa na lengo la kuhamashisha utamanduni wa kuweka akiba kwa wateja wa Timiza Akiba na vile vile kuwavutia wateja wengine wapya. Tunaendelea kutoa wito kwa Watanzania kuendeleakujenga utamanduni wa kuweka akiba alisema Nchunda huku akiongeza kuwa AirtelTanzania imeshirikiana na benki ya Letshego kuendesha kampeni hii”.
Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Letshego Mbajo Pius Mchomvu akimkabidhi mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Nigwike Kibona ambaye ailijishindia Tzs 1 milioni. Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ya wiki sita ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kuwa na utamanduni wa kujiwekea Akiba huku ikiendesha kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania na benki Letshego. Kati kati ni Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Plc Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Emmanuel Lugakingira ambaye ailijishindia Tzs 5 milioni. Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ya wiki sita ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kuwa na utamanduni wa kujiwekea Akiba huku ikiendesha kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania na benki Letshego. Kati kati Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Letshego Mbajo Pius Mchomvu.
Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Plc Jackson Mmbando (katikati), akimtambulisha mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Emmanuel Lugakingira ambaye ailijishindia Tzs 5 milioni kwa Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Letshego Mbajo Pius Mchomvu mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake leo jijini Dar es Salaam. Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ya wiki sita ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kuwa na utamanduni wa kujiwekea Akiba huku ikiendesha kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania na benki Letshego.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad