Maneno hayo yalisemwa (kwa tafsiri isiyo rasmi) na Balozi wa Marekani nchini Tz. Dr. Donald Wright wakati alipitembelea Mkomazi kwa siku mbili. Aitabiria Mkomazi kuja kuwa kati ya mbuga bora zenye kupendwa.
Afurahishwa na kuona Faru kwa karibu kitu ambacho amekiri hajawahi kuona hivyo kabla.
Aahidi kushirikiana na Wilaya/TANAPA kutatua migogoro kati wa wanyama na binadamu hasa Tembo wanaoingia kwenye maeneo ya wananchi. Pia maeneo ya afya hasa kwa kuwa yeye ni Daktari.
Aahidi kuleta watalii na wawekezaji pia kurudi tena Mkomazi- Same.
Akipokea kumbukumbu toka kwa DC Same afurahia kalenda yenye maneno
" Same is not the same "





No comments:
Post a Comment