Mkurugenzi
wa kituo cha Uvumbuzi na Ujasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Dkt. Ambrose Itika ambaye alikiwa mgeni rasmi katika kilele cha utowaji
Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur awards -
GSEA) (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Tuzo
hiyo ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza,
Denis David (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Mratibu Mkuu
wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur
awards - GSEA), Emir Karamagi, Rais na Mratibu wa Tuzo za Ujasiriamali
kwa Wanafunzi hapa nchini, Rajabu Katunda pamoja na Mkuu wa Rasilimali
Watu wa Karimjee Jivanjee Group, Janet Lekashingo. Wanafunzi wa vyuo
mbalimbali nchini walishindanishwa katika ubunifu wa ujasiriamali na
Denis David akaibuka mshindi kwa ubunifu wake wa kuhifadhi mazingira kwa
kuokota Nywele katika saluni za vinyozi mbalimbali na kutengeneza
Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea Viwatilifu vinavyouwa magugu
mashambani, ambapo amejipatia kiasi cha dola za Kimarekazi 1000 (Elfu
moja) zitakazomsaidia katika kuendeleza ubunifu wake.
Mshindi
wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur
awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa
kwanza, Denis David akizungmza na kutoa shukrani kwa waandaaji wa tuzo
hizo mara baada ya kuibuka Mshindi katika kilele cha mashindano hayo
yaliyowakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Denis David kaibuka mshindi kwa
ubunifu wake wa kuhifadhi mazingira kwa kuokota Nywele katika saluni za
vinyozi mbalimbali na kutengeneza Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea
Viwatilifu vinavyouwa magugu mashambani, ambapo amejipatia kiasi cha
dola za Kimarekazi 1000 (Elfu moja) zitakazomsaidia katika kuendeleza
ubunifu wake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Cool Blue Limited akizungumza wakati wa
hitimisho la shindano la Global Student Entrepreneur awards (GSEA)
lililoshirikisha wanachuo wajasiriamali hapa nchini.
Mshehereshaji
Miranda Naiman akizungmza wakati wa hitimisho la Shindano la Global
Student Entrepreneur awards (GSEA), lililofanyika jijini Dar es Salaam
na Denis David kuibuka Mshindi wa shindano hilo.
Mshindi
wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur
awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa
kwanza, Denis David akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake.
Mshindi
wa Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi (Global Student Entrepreneur
awards - GSEA) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa mwaka wa
kwanza, Denis David akiwa katika picha ya Pamoja na waandaaji wa
shindano la Global Student Entrepreneur awards (GSEA) pamoja na majaji.
========= =========
MSHIRIKI wa shindano la kuwania Tuzo za Ujasiriamali kwa Wanafunzi Ulimwenguni (Global
Student Entrepreneur awards - GSEA), David Denis aibuka kidedea katika
shindano hilo lililoshirikisha wajasiliamali vijana na wanafunzi wa vyuo
mbalimbali hapa nchini.
Shindano
hilo lilishindaniwa na wengi lakini tamati ya mashindano hayo walipata
washiriki watano ambao ni Upendo Ngusa, Mwaki Mashy, Balbina Gulam,
David Denis, Adam Duma ambapo kila mmoja alipata nafasi ya kuelezea
wanachokifanya na jinsi walivyoajiri vijana katika miradi wao hiyo.
Akizungumza
wakati wa mashindano hayo Mkurugenzi wa kituo cha Uvumbuzi na
Ujasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ambrose Itika alisema
kuwa washiriki wa shindano hilo wanatakiwa wajikite zaidi katika ubora
wa bidhaa zitakazo saidia jamii zaidi ili kuendelea kulinda mazingira
nchini.
"Mmeonesha ujuzi wenu hapa sasa nendeni
mkauendeleze ili kuleta matokeo mazuri zaidi na kuleta manufaa katika
jamii zetu bila kuharibu amani ya nchi yetu huku mkifanya kazi na watu
tofauti tofauti kwa kujiletea faida katika miradi yenu ya maendeleo."
Amesema Dkt. Itika
Kwa upande wake Mshindi wa
shindano la GSEA na Mkurugenzi wa taasisi ya Cutoff Recycle, Denis David
amewashukuru waanzilishi wa Mashindano hayo kwani yamekuwa yakiibua na
kuwafunza watu wengine pamoja na kutatua changamoto katika jamii
inayowazunguka.
Denis amesema kuwa ushindi huo
si wake peke yake bali ni wa kila mfanyakazi wa kampuni yake ya Cutoff
Recycle na kwa wale watunza mazingira wote kwa kutumia kutengeneza
bidhaa mbalimbali kwa kutumia takataka.
Mshindi
wa shindano hilo, Denisi aliyetokea Arusha na Mwanachuo wa Chuo Kikuu
cha Ardhi kwa mwaka wa kwanza amesema kuwa ubunifi wake ni wa kuhifadhi
mazingira kwa kuokota Nywele katika saluni za vinyozi mbalimbali Mkoani
Arusha na kutengeneza Mbolea ya Maji pamoja na kutengenezea Viwatilifu
vinavyouwa magugu mashambani.
"Sisi tunafika
kwenye saluni ili kuhakikisha nywele hazitupwi kwenye dampo kwani
zitazidi kuongeza uchafu kule baada ya kukusanya nyingi tunazibadilisha
zile nywele halisi za bianadamu na kuwa mbolea ya kimiminika." Amesema
Denis
Amesema kuwa nywele halisi za binadamu
zinaweza kutengeneza viwatilifu ambavyo vinauwa magugu shambani na
zimeweza kusaidia kutuza mazingira.
"Tunatengeneza
bidhaa ambazo ni rahisi kwa matumizi huku tukizingatia utunzaji wa
mazingira kwa kutengeneza bidhaa zinazoweza kutumika tena huku tukiajili
kundi la vijana." Amesema Denis
Hata hivyo
ameiomba serikali kutembelea wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanaotumia
takataka kutengeneza bidhaa nyingine kwa kusaidia kutunza mazingira
yetu.
Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila
mwaka ikiwa kwa mwaka 2019/2020 Moses Katala aliibuka mshindi na
kujinyakulia kitita cha shilingi milioni Moja. Na mashindano ya
2020/2021 David Denis amejipatia dola za Kimarekazi 1000 (Elfu moja) kwa
kuibuka mshindi wa shindano la GSEA.








No comments:
Post a Comment