Baadhi
ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB ambao wapo katika Klabu ya wakimbiaji
ya Benki hiyo (CRDB Jogging Club) wakiwa katika picha ya pamoja wakati
madhimisho ya mwaka mmoja wa klabu ya wakimbiaji ya Kigamboni.
Na Mwandishi wetu.
Kuelekea
mbio za hisani za Benki ya CRDB "CRDB Bank Marathon", klabu ya
wakimbiaji ya Benki ya CRDB imeendelea kufanya mazoezi na uhamasishaji
kwa wakimbiaji na watu mbalimbali kujitokeza kushiriki katika mbio hizo
ambazo zina lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji kwa
watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Benki ya
CRDB, Emmanuel Kiondo alisema ushiriki wa klabu hiyo ni katika
maazimisho hayo ni sehemu ya uhamsishaji wa jamii kujitokeza kwa wingi
kuchangia matibabu kwa watoto hao wenye magonjwa ya moyo.
"Watoto
zaidi ya 500 wanasuburia matibabu ya upasuaji wa moyo katika Taaisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete. Ni wajibu wetu sisi kama Watanzania kujitokeza
kwa wingi kuwasaidia kupitia CRDB Bank Marathon."
Akielezea
namna ya kujisajili na kushiriki katika CRDB Bank Marathon, Kiondo
alisema washiriki wanatakiwa kutembelea tovuti maalum ya
crdbtz.co/marathon na kisha kufuata hatua chache za kujisajili kwa mtu
binafsi na vikundi.
“Kujisajili
ni rahisi sana, unaweza kujisajili binafsi na kuchangia shilingi
30,000 au kupitia vikundi na kuchangia 25,000 kwa kila mmoja kupitia
matawi ya Benki ya CRDB, CRDB Wakala, SimBanking App na mitandao ya
simu (M-Pesa, TigoPesa, AirtelMoney). Fedha hizi zote zitaelekezwa
katika kusaidia gharama za upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo,”
alisema Kiondo.









No comments:
Post a Comment