JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Mkemia Mkuu wa Serikali:Uchunguzi wa vinasaba matokeo kupatikana ndani ya Siku 21

Share This
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja waandishi katika mafunzo ya waandishi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKEMIA Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika maabara ya mamlaka hiyo hufanyika ndani ya siku 21 pekee na sio zaidi ya hapo huku gharama ya uchunguzi huo wa vinasaba ikiwa ni shilingi laki moja kwa kila sampuli.

Akizungumza leo wakati akifunga mafunzo  maalumu ya siku mbili kwa waandishi wa habari jijini Dar esSalaam yaliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya majukumu ya mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali (GCLA)

"Ni siku 21 pekee ndizo zinazotumika kuchunguza vinasaba mbalimbali na sio zaidi ya hapo labda itokee janga la dharura kama lile la moto Morogoro  ambalo ilitulazimu kutumia siku kumi usiku na mchana kwa kufuata hatua zote ili kupata vinasaba na kuweza kuwapumzisha wapendwa wetu." Ameeleza  Dkt. Mafumiko.

Aidha Dkt.Mafumiko amesema kuwa mamlaka hiyo ina dawati la malalamiko ambalo lipo wazi wakati wote kuwahudumia wananchi na amesisitiza kuwa huduma zote za kiuchunguzi wa kimaabara kutoka katika mamlaka hiyo zinatoka kwa vibali maalumu kwa kuzingatia sheria na kanuni.

Mkurugenzi wa idara ya sayansi, jinai na vinasaba (DNA), Khadija Mwema amesema kuwa uchunguzi huo hufanywa na makundi mbalimbali kwa kuwahusisha madaktari wenye sifa na waliosajiliwa na kutambulika na Serikali, wakemia wenye sifa na askari wa jeshi la polisi kuanzia ngazi ya Inspekta na hufanywa kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu.

Mwema ameeleza kuwa majukumu ya mamlaka hiyo  yamegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni uchunguzi wa kimaabara wa sampuli na vielelezo mbalimbali, utekelezaji wa sheria tatu ambazo mamlaka hiyo inazisimamia pamoja  na kutoa ushahidi wa kitalaamu kwenye masuala yanayohusu uchunguzi wa kimaabara katika  mahakama mbalimbali nchini.

Mamlaka hiyo ambayo ni maabara ya rufaa ilyoanza mwaka 1895 na kuwekeza zaidi katika mitambo, wataalamu na kuimarisha maabara katika kanda zote sita imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia afya, haki, amani na utulivu kote nchini.

Mwandishi mwandamizi kutoka Michuzi Blog, Chalila Kibuda  kwa niaba ya waandishi ameiomba mamlaka hiyo kuendelea kutoa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo zaidi wa kuandika kwa mapana na kwa weledi kuhusiana na mamlaka hiyo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Mamlaka hiyo imekutana na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali zaidi ya 100 ambao wamepata nafasi ya kufahamu kwa kina zaidi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo.


 Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Bidhaa wa Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Sabanito Mtega akitoa mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya mamlaka hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkrugenzi wa Idara SayansiJinai na Vinasaba wa Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Khadija Mwema akitoa jinsi ya taratibu za kuomba uchunguzi katika maabara ya Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika  mafunzo ya waandishi wa habari  mamlaka hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugunzi wa Idara ya Usimamizi  wa Kemikali wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo akitoa maalezo kwa waandishi wa habari namna wanavyosimamia kemikali na sheria zinazotumikuingiza nchini kukiwepo na mikataba mbalimbali ya Kemikali katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Sehemu  ya waandishi wa katika mafunzo ya maamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari wakati akifunga mafunzo ya waandishi habari yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Michuzi Media Group (MMG) Chalila Kibuda akitoa neno shukrani kwa niaba ya waandishi walioshiriki mafunzo ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad