WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kufanya nchi hii kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuendelea kusimamia mawazo wa aliyekuwa Rais wa kwanza nchini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, William Tata Ole Nasha alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius .K. Nyerere lilifanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mtazamo wake wa kuanzisha ,kuendeleza na kudumisha viwanda vya ndani ya nchi kukidhi mahitaji ya wananchi pasipo kutegemea Zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi .uthubutu wa kuanzisha Viwanda vya nguo kama vile Kiwanda cha Urafiki ,Mwatex , Mbeyatex na Mutex ni hatua inayokisi mtazamo wake juu ya Viwanda.” Amesema Ole Nasha.
Amesema hivyo kwa namna ya pekee nimpongeze Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavyosimamia utekelezaji wa mpango huu kwanza kwa kurejesha maadili kwa viongozi na kusimamia matumizi ya rasilimali bora za nchi.
Kwa upande wake mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Prof. Shadrack Mwakalila amesema Baba wa Taifa alisema Julai 29 mwaka 1961 wakati wa ufunguzi wa chuo hicho kuwa alisema kuwa wale wote watakaopata nafasi ya kusoma na kufuzu kivukoni watafanana ma hamira katika mkate. Haiwezekani kutenga hamira katika mkate bali tunajua hamira ipo kwa kutazama jinsi ilivyomua mkate.


No comments:
Post a Comment