Mkurugenzi wa
Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS),
Epharaim Kwesigabo
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusianaMfumuko wa bei wa Mwezi Agosti Mwaka huu(2017) kwa kipimo cha
Mwezi umepungua kwa asilimia 0.4
Mkurugenzi wa
Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo
jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti
Mwaka huu.Kulia ni Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2017 umepungua zaidi hadi kufikia asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai2017.
Hayo
ameyasema Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na
Makazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema hii
inamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa
mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na
kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai,2017.
Kwesigabo alisema Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 8.6 kutoka asilimia 8.9 ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.
"Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.46 mwezi Agosti, 2017 kutoka 103.28 mwezi Agosti, 2016" alisema Kwesigabo.
Akizungumzia
mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na
migahawani kwa mwezi Agosti,2017 umepungua hadi asimilia 9.1 kutoka
asilimia 9.3 mwezi Julai 2017. Ambapo badiliko la Fahirisi za bei zisizo
za vyakula umebaki kuwa asilimia 3.1 mwezi Agosti, 2017 kama ilivyokuwa
mwezi Julai, 2017.
Kwesigabo
ameongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa
mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.2
Julai, 2017.
Fahirisi inayotumika kukokota aina hii ya mfumuko wa bei haijumuishi
vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petroli,
dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa kuni na umeme.
Amesema vyakula na bidhaa za nishati vinasifa ya kuwa na bei ambazo hubadilika
mara kwa mara, hivyo vikiondolewa kwenye fahirisi ya bidhaa na huduma
zote hubakia fahirisi ambayo ina mwelekeo imara kwa watunga sera.





No comments:
Post a Comment