Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde akifafanua jambo wakati wa kufungua
dirisha jipya litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi kuweza
kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. katikati ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dkt. Fred Msemwa na kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Maryjene Makawia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dkt. Fred Msemwa na kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Maryjene Makawia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dkt. Fred Msemwa (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufungua
dirisha jipya litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi kuweza
kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde na Kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Maryjene Makawia.
kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Maryjene Makawia akizungumza na waandishi wa ahabari jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dkt. Fred Msemwa.
Kulia ni Afisa Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Irene Kasanda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dkt. Fred Msemw na Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Maryjene Makawia.
Picha na Avila Kakingo, Blog ya Jamii.
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
WATUMISHI
Housing Company (WHC), wamefungua dirisha jipya litakalowezesha
watumishi wa sekta binafsi kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu
na kuwainua kiuchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
WHC, Dkt. Fred Msemwa, amesema, dirisha hilo ambalo litajumuisha
Watumishi wote wale wa umma na wa binafsi, litawawezesha wafanyakazi
wote kuwa na makazi bora kupitia umiliki wa nyumba kwani nyumba hizo
wanaweza kuzitumia kwa kukopa kuanzisha miradi mbali mbali ya uchumi.
Amesema
Watumishi hao wa sekta binafsi ambao nao wanapata fursa ya kununua
nyumba hizo ni wale ambao hawako katika utumishi wa umma lakini
wanachangia katika mifuko ya pensheni.
Ameongeza
kuwa, wigo huo mdogo unatokana na mahitaji ya wengi kwani watu wengi
ukitoa Watumishi wa umma ambao hapo awali ndio walikuwa na sifa ya
kununua nyumba hizo,wanashida ya makazi bora na ya kisasa
"Kufuatia
uamuzi huu, WHC sasa itakuwa ikiwahudumia Watumishi wa umma pamoja na
wafanyakazi wengine walioko katika sekta binafsi ikiwa ni muendelezo wa
juhudi za Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuwawezesha
wafanyakazi wote kuwa na makazi bora na kuwainua kiuchumi kupitia
umiliki wa nyumba", amesema Dkt Msemwa.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha mauzo na masoko wa WHC, Raphael Mwabuponde
amewaalika watanzania wote wenye uhitaji wa nyumba hizo, kutuma maombi
kwa kuchukua fomu katika tovuti ya WWW.whctz.org.
Ameongeza
mpaka sasa bado kuna nyumba za kuuza zilizopo Bunji B, Gezaulole
Kigamboni, Mkundi Morogoro, Mwanza Kisesa na Njedengwa Dodoma.
No comments:
Post a Comment