Wachezaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC,
wakishangilia ushindi wao baada ya kuiadhibu timu ya wafanyakazi wa
Huawei mabao 7-1 wakati wa mchezo wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa
wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji hatari wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao
akifunga goli wakati wa mchezo wa kirafiki na Kampuni ya Huawei
uliofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam.Vodacom Tanzania PLC iliibuka na ushindi wa magoli 7-1.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (jezi no.9) na
nahodha wa timu ya kampuni hiyo, Ngayama Matongo (wapili kushoto)
wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya kampuni ya Huawei wakati wa
mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc
ilishinda magoli 7-1
Mshambuliaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, (kushoto)
Astrid Mapunda akimtoka beki wa timu ya wafanyakazi wa Huawei , wakati
wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo, uliofanyika mwishoni mwa
wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania
Plc ilishinda magoli 7-1.
Kikosi cha timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ian Ferrao(katikati) aliyeshika mpira wakipozi kwenye picha kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya kampuni ya Huawei uliofanyika kwenye viwanjwa vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Vodacom Tanzania iliilaza Huawei magoli 7-1.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Mengdong Gao,(kulia) akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, Ngayama Matongo (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1.
Mabeki wa timu ya Vodacom Tanzania PLC wakimdhibiti mshambuliaji wa timu
ya Huawei, Li Kun , wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,
uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam, Vodacom Tanzania iliibuka kidedea kwa magoli 7-1
Wachezaji wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, wakipeana mbinu za ushindi
wakati wa mapumziko ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi
wa kampuni ya Huawei, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya
Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania PLC, ilishinda magoli
7-1
Mfungaji bora wa mechi ya kirafiki kati ya Vodacom Tanzania PLC
na Huawei,Kungwi Michael akionesha kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora
na kikombe mara baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo
uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam, Vodacom Tanzania, ilishinda magoli 7-1.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Huawei Mengdong Gao (kulia) akimkabidhi
mchezaji wa timu ya Vodacom Tanzania PLC, Kungwi Michael tuzo ya
ufungaji bora baada ya mchezo wa kirafiki baina ya kampuni
hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini
Dar es Salaam, Vodacom Tanzania, ilishinda magoli 7-1 . Kushoto ni
nahodha wa timu hiyo, Ngayama Matongo.
No comments:
Post a Comment