Mkuu
wa Operesheni wa Hospitali ya Aga Khan, Sisau Konte akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na namna
wanatakavyofanya upasuaji wa Viungo vilivyokakamaa kutokana na ajali za
moto pamoja na ajali za barabarani. Kulia ni Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Upasuaji, Athar Ali.

Meneja
masoko na Mawasiliano wa Hospitali ya Aga Khan, Olayce Lotha akifafanua
jambo mblele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya
upasuaji wa viungo vilivyokakamaa utakao kuwa unafanyika katika
hospitali ya Aga Khani jijini Dar es Salaam wajitokeze kwani matibabu
hayo yatakuwa hayana gharama yeyote upasuaji utakaoaza Novemba 3hadi 5
mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
HOSPITALI
ya Aga Khan hapa nchini imeeandaa mpango maalumu kwaajili ya upasuaji
wa viungo vilivyokakamaa kutokana na ajali za moto, ajali za barabarani
pamoja na ukatili naofanyika majumbani upasuaji huo utaanza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa mpango huo utaaza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu katika
hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaa na kwa wakazi wa Mikoani
waweze kujisajili katika Hospitali yeyote ya Aga Khani na wanaoweza
kusafiri na kufika katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam ambako
kunatolewa hiyo huduma.
No comments:
Post a Comment