WIZARA ya afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa Tanzania(MSD)
wamesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Zipline jijini Dar es
Salaam leo kwaajili ya kuanza kujenga vituo vya kurushia Drone za
kusafirishia dawa kataka maeneo mbalimbali hapa nchini wakianzia na Mkoa
wa Dodoma na Mwanza.
akizungumza
wakati wa kusaini na kubadilishana mikataba ya makubaliano, Katibu Mkuu
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki
Ulisubisya amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka kutokana na
ukuaji wa Teknolojia Bohari ya Dawa Tazania itapata urahisi wa kusambaza
zawa katika vituo mbalimbali vya Afya.
Amesema
kuwa kwa kuanza mradi huo utaanza kwa kusambaza dawa ambazo
zinaubaridi kama Damu katika vituo 200 vya mkoa wa Dodoma ambapo baada
ya hapo watandelea na mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae nchi nzima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo,amesema kuwa
Mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini Rwanda na hapa nchini
utaenda vyema zaidi pia amesema kuwa utatoa ajira nyingi kwa vijana wa
kitanzania ambao watakuwa na mawazo mazuri ya ubunifu kwaajili ya
kuendeleza kuenea mradi huo hapa nchini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.
Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa kusaini Mkataba kati ya wizara ya
Afya, Bohari ya Dawa Taznania(MSD)
na Kampuni ya Zipline kwaajili ya kuanza kufanya utafiti wa maeneo
yatakayojengwa kwaajili ya sehemu ambapo Kampuni ya Zipline itakuwa
ikirushia vifaa maalum ambazo ni Drone zitatumika kusambaza dawa katika
mikoa maeneo ambayo ni ngumu kufikika kwa urahisi kutokana na umbali
wake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo, akizungumza wakati wa
kusaini Mkataba wa Makubaliano kuanza kujenga vituo kwaajili ya kurushia
Drone ambazo zitakuwa zikisafirisa dawa kwenye maeneo ambayo hayafikiki
kwa urahisi ikiwa mradi huo utaanza katika mikoa ya Dodoma na Mwanza.
Katikati ni Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo wakisaini mkataba wa kuanza
kujenga vituo vya kurushia Drone zitakazo kuwa zikisafirisha dawa kwenye
maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali,
Profesa Bakari Kambi.
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu wakibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo wakibadilishana kwaajili
ya kuanza kujenga vituo vya kurushia drone zitakazo kuwa zikisafirisha
dawa katika maeneo mbalimbali ya nchi. Ktikati ni Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.
Mpoki Ulisubisya akisuhudia wanavyobadilishana mikataba hiyo jijini Dar
es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment