Mkurugenzi
wa Kampuni ya Max Com Africa Juma Rajabu akimuonyesha Mwenyekiti wa
kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia namna ya mfumo wa kutumia kadi
unavyo fanya kazi katika vituo vya Mabasi yaendayo haraka katika kituo
cha Mabasi ya haraka cha Feri jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia, akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa haabari juu ya ziara yao ya kutembelea mradi wa ukusanyaji
fedha katika kituo cha Feri cha mabasi yaendayo Haraka
Mbunge
wa Ileje na mjumbe wa Kamati ya Bajeti, Janeth Mbene akipanchi tiketi
katika kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Feri Jijini Dar es
Salaam wakati wajumbe wa kamati hiyo ilipotembelea miradi ya Maxcom
Africa
Mbunge wa Rombo , Joseph Selasini akipanchi tiketi katika kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Feri
Jijini Dar es Salaam wakati wajumbe wa kamati hiyo ilipotembelea miradi
ya Maxcom Africa
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari
Akifafanua Jambo kwa wabunge wa kamati ya Bajeti walipotembelea Mradi
wa ukusanyaji mapato wa Max Malipo katika Vituo vya Mabasi ya Endayo
Haraka
Kaimu Mtendaji Mkuu DART, Ronald Lwakatare, akifafanua
Jambo kwa wabunge wa kamati ya Bajeti walipotembelea Mradi wa
ukusanyaji mapato wa Max Malipo katika Vituo vya Mabasi ya Endayo Haraka.
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania na Wajumbe wa kamati ya
Bajeti wakiangalia miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo harakajijini
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment