jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

WHITE RIBBON ALLIANCE YAOMBA WIZARA YA FEDHA KUONGEZA BAJETI YA HUDUMA ZA UZAZI WA DHARURA.

Share This
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WIZARA ya Fedha na Mipango yaombwa kuongeza Bajeti ya huduma za uzazi za Dharura hadi kufikia asilimia 100 ili kuokoa maisha ya kinamama na watoto wa changa wakati wa kujifungua.

Ameyasema hayo Mratibu wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay  wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa Serikali iweke wigo wa fedha zinazopangwa kwaajili ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi isitumike kwa shughuli nyingine.

Rose amesema kuwa Vifo vitokanavyo na uzazi havivumiliki, wilaya zote za kila mkoa ziweke kipengele cha huduma kamili za uzazi za dharura (CEmoNC) ili kuondokana na vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa vifo vingi vya akina mama na watoto vinatokana na mambo mbalimbali hasa ukosefu wa huduma kamili za Uzazi za dharura  katika hospitali, upungufu wa Damu salama na kuwa na wakunga wasio na ujuzi katika hospitali.

Mtoa Maada na Mshauri wa Maswala ya Habari, Chiku Lweno akitoa maada kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0644
 Mratibu wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa mafunzo juu ya kutokomeza Vifo vya akinamama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.
DSC_0667
 Meneja Mtetezi wa Mradi wa The White Ribbon Alliance, Sizarina Hamisi akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0693
DSC_0698
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mafunzo hayo yaliyotolewa na wafanyakazi wa White Eibbon Allince jijini Dar es Salaam leo.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad