Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura akiwakabidhi wachezaji bendera ya Taifa kwaajili ya kwenda kupeperusha huko Rio De Jeneiro nchini Brazil wanaokwenda kushiriki mashindano Olimpiki.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi akizungumza kabla ya kukabidhi bendera na kuwaaga kwa wanaokwenda katika mashindano ya Olimpiki Rio De Jeneiro nchini Brazil.
Baadhi ya wadau wa michezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa mashindano ya Olimpiki wanaoenda nchini Brazil
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura
amewataka washiriki wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya
Olimpiki mwaka huu Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha
wanafanya vizuri ili kurudi na medali, hayo ameyasema wakati wa
kukabidhi bendera kwa timu za kuogelea, judo na riadha leo Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es salaam.
Wambura
amesema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya
watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza
kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao. "
Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki na macho yote ya watanzania
yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na
medali zeni kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya
ushindi".
Akiwa
anawakabidhi bendera hiyo, Wambura amewaasa wanamichezo hao kutumia
fursa nyingine ya kujifunza zaidi kwani kama wataenda kukutana na
mataifa mengine mbalimbali. Naye moja ya wadhamini wa safaru hiyo
kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi
kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao
zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.
Mkurugenzi
wa Multichoice Maharage Chande amesema mwaka huu mashindano yote
yatakuwa yanakuja moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na
itawapa fursa watanzania kuwashuhudia.wawakilishi wao kwenye mashindano
hayo makubwa duniani. Mbali na hilo watakapokuwa huko waitangaze nchi
yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili kuzidi kupata watalii mbalimbali
kutoka.kote duniani hayo yamesemwa na Godfrey Tengeneza mkurugenzi wa
utalii nchini.
Katibu
Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi amesema kuwa kwa
mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na
wengine wakiwa nje ya nchi na hilo.limefanikisha kuweza kujifua vyema
ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani. Hilal ameweza kuweka kambi nchini
Dubai, Magdalena alikuwa nchini Australia. Andrew aliweka kambi chuo
cha polisi Moshi na wanariadha waliweka kambi mkoa wa Arusha.
Washiriki
kwa upande wa riadha ni Alphonce Simbu, Said Makula l, Fabian Naasi na
Sarah Makela. Timu ya kuogelea inawakilishwa na Hilal Hilal na Magdalena
Moshi na Judo ni Andrew Mlungu. Huku timu ya kwanza ikitarajiwa
kuondoka alfajiri ya leo wakiambatana na daktari wa timu Nasoro Matuzya.
No comments:
Post a Comment