JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ASILIMIA 51 YA WATOTO WA UMRI 0 HADI 6 MIEZI HUNYONYESHWA MAZIWA YA MAMA PEKEE- DK.KIGWANGALA.

Share This
 Mkurugenzi wa Msaidizi wa kitengo cha Uzazi na Afya ya Mtoto wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto , Dk Georgina Msemo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dra es Salaam leo kuhusiana na chakula cha mtoto wa kuanzia mwezi sifuri hadi sita kuwa ni maziwa ya mama pekee na sio kumpa chakula kingine. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Lishe wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Vincent Assey na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Sabas Kimboka.
Mtafiti Msaidizi wa Maswala ya Lishe, Mary Msangi (Aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana ya likizo ya Mama aliyejifungua na baba mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
UTAFITI unaonyesha ni asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi sifuri (0) hadi miezi sita (6) wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa chakula kingine na asilimia 41 ya watoto hao hawanyonyeshwi ipasavyo kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya hivyo watoto wako katika hatari ya kupata utapiamlo na magonjwa yanayotokana na ulishaji usiofaa
 kutokakana kadri ya inavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi wa Msaidizi wa kitengo cha Uzazi na Afya ya Mtoto wa Wizara ya Afya, ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto , Dk Georgina Msemo kwa niaba  ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wakati wa kutangaza maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo hufanyika kila Agasti 1 hadi 8, amesema  kuwa kiwango hicho kinatakiwa kuongezeka kwa akina mama kunyonyesha ili kuweza kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs).

Amesema kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo elimu inahitajika katika kuelimisha suala la unyonyeshaji ili kuweza kuandaa kizazi chenye afya ya mwili na akili kwa maendeleo ya taifa.

Dk. Georgina amesema watoto wakinyonyeshwa kwa ushauri wataalam wa afya wanakuwa na akili ambayo inakuwa imechangiwa na maziwa ya mama.

Aidha amesema kuwa  malengo ya maendeleo endelevu yanahusiano na unyonyeshaji katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na lishe, uhakika wa  chakula na kupunguza umasikini.

Kilele cha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Kagera ambapo elimu hiyo itaendelea kutolewa nchi nzima lengo ni kuweza kuwa na watoto wasio na utapiamlo kutokana na kula au kunyonyeshwa bila kufuata utaratibu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad