Wananchi wa kijiji cha Lupondo,kata ya mkamba wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Abdallah ulega katika mkutano wake wakuwashuruku wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo huku akihaidi kutoawaangusha nakwamba atakuwa karibu na watu wake.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibunguchana,kata ya mkamba ikiwa ni sehemu ya utaratibu ambao ameuweka wa kwenda kushukuru,na kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo leo katiaka kijiji cha kibunguchana mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kibunguchana, Ahamad Mbonde akizungumza maneno yaufunguzi kabla ya kumkaribisha mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega kuzungumza na wananchi hao leo mkoani Pwani.
Mbunge ulega wajimbo la Mkuranga akihesabu fedha.
Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi fedha taslimu shilingi laki tatu kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Kibunguchana, Ahamad Mbonde kwa ajili ya kuazisha msingi wa ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo ambapo pia alifanya harambee ndogo iliyowashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo akiwa Mwenyekiti wa halmashauri, Juma abed ambaye alichangia mifuko kumi yacementi na diwani wa kata hiyo Hassan Dunda alichangia pia mifuko kumi ya cementi leo mkoani Pwani.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Mwandishi wetu.
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amewataka vijana wa Wilaya hiyo kujiunga katika vikundi vya vikoba vinavyoazishwa kwenye maeneo yao na kwamba wastarajie kuwa ahadi ya rais ya kutoa sh. Milioni50 kila kijijihaitaenda kwa mtu mmoja mmoja bali kwa kukaa katika makundi.
Amesema kuwa kama wananchi wanataka fedha hizo ziwafikie lazima wakae kwenye vikundi na si vinginevyo ,huku akisisitiza akina baba nao kuacha kutumia muda wao mwingi kucheza bao badala yake wajiunge katika vikundi.
Ulega ametoa wito huo jimbo humo wakati akizungumza na wanachama wa kikundi cha Vikoba cha Tuamke kilichopo katika kijiji cha Lupondo kata ya mkamba.
Alisema kuwa hakuna namna kwani maendeleo yanakuja Kwa kukaa katika vikundi mbalimbali na hata fedha za rais zitaelekezwa katika vikundi hivyo,hivyo kazima watanzania wachangamkie fursa hiyo.
"Binafsi Leo nawachangia sh.laki tatu kwani mmeonesha dhamira ya dhati kupitia risala yenu ambayo mmesoma mbele yangu nami nahaidi nitakuwa pamoja nami kamwe si tawaacha."alisema Ulega.
Aidha alisema kuwa yeye kama mbunge kuna mipango mingi ambayo anayo Kwa ajili ya watu wake ikiwa pamoja na kuleta watu wenye makampuni ya Pikipiki ili kuja katika wilaya hiyo na kukopesha vijana Pikipiki hizo na baadae kulipa kidogokidogo Kwa muda wa miezi 11.
Alisema kuwa lazima vijana,akina baba na akina mama Kwa pamoja wakubali kutengeneza vikundi vya vikoba kwani fursa nyingi zinapitia katika vikoba na si Kwa mtu mmoja mmoja.
Aidha Ulega akiwa katika ziara ya kijiji cha Lupondo alipata fursa ya kufungua jengo la Tuamke Vikoba ambapo pia alitembelea Zahanati ya Kijiji hicho nakuhaidi kutatua tatizo la miundombinu ya Maji.
Alisema kuwa anatambua kuwa Zahanati hiyo inachangamoto kubwa ya Maji hivyo atahakaikisha anasimamia ujenzi wa kisima pamoja na kuona Zahanati hiyo inapata umeme wa Tanesco Kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma.
"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu wote kuleta umeme hapa na kama ule wa tanesco utachelewa basi nitahakikisha naleta solar hapa."alisema Ulega.
Pia mbunge huyo alisema kuwa wananchi watambue kuwa yupo Kwa ajili yao na kwamba watakuwa pamoja katika kipindi chonde cha uongozi wake ikiwa pamoja na kuhakikisha anasukuma huduma jwa wananchi wake.
Naye Diwani wa Kata Dundani ,Hassan Dunda aliwaeleza wananchi hao kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi huku akisisitiza kuwa watu kukaa katika makundi Kwa ajili kupata mikopo.
Ulega mbali na kufanya ziara katika kijiji cha Kupondo pia alitembelea vijiji vingine mbalimbali ndani ya Kata ya Mkamba ,ambapo pia anaendelea na ziara hizo za kutoa shukrani na kukagua miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment