Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam VETA imetoa vifaa vya thamani ya sh.milioni 11 katika atamizi ya Osarika Woodwork ikiwa ni sehemu ya kuendeleza atamizi hiyo kwa ujuzi na kufundisha vijana wengine wanaoenda kufanya mafunzo ya vitendo.
Akizungumza leo wakati hafla ya kukabidhi vifaa katika atamizi ya Osarika Woodwork, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko amesema kuwa vifaa hivyo walivyotoa kwa kikundi hicho kuongeza uzalishaji samani mbalimbali ikiwa ni pamoja kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaotoka Veta.
Amesema vijana wa Osarika ni zao la VETA ambao wameweza kuunda kukundi na kusajili hivyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira lakini wameonyesha njia mpaka kuja kuongeza nguvu ya vifaa.
Bukko amesema vifaa hivyo ni mali kikundi cha Osarika wakivurugana vitu hivyo wanatakiwa kurudisha ili vikaweze kufanya kazi katika atamizi nyingine .
Aidha amesema kuwa VETA kuendeleza ni atamizi ni sehemu yao katika kuhakikisha atamizi zinaendelea katika kuzalisha ajira za vijana kutokana na mafunzo waliopata katika vyuo vya Ufundi.
Naye Mwakilishi wa Diwani wa Kata ya Tandika, Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Mabatini ,Sharifu Jumbe amesema kuwa vijana wanatakiwa kujituma katika kufanya kazi na kuwataka wengine waende kupata mafunzo VETA.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabidhi moja ya kifaa cha Kukatia Mbao na Alminium mwanaatamizi ya Orasika-Tandika, David Mshilili jijini Dar es Salaam leo. Kulia aliyevaa Koti ni Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habibu Bukko.
Sehemu ya misaada ya iliyotolewa na chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam leo katika kikundi cha Atamizi ya Orasika iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuongeza nguvu kwa vijana ili kupunguza ongezeko la vijana wasio na ajira.
Mtafiti mwandamizi wa Soko la Ajira VETA, Peter Katabi akitambulisha viongozi mbalimbali wa chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi wanakikundi cha Atamizi ya Osarika vifaa vya ufundi vyenye thamani ya shilingi Milioni 11 kutoka VETA jijini Dar es Salaam leo.
Fundi wa Atamizi ya Osarika kilichopo Mtaa wa Magulue-Tandika jijini Dar es Salaam,Salum Sese akizungumza kwa niaba ya wanakikundi cha atamizi ya Osarika jijini Dar es Salaam leo.
Fundi wa Atamizi ya Osarika, Zadoki James akisoma risala kwa niaba ya kikundi cha Atamizi ya Osarika kabla ya kupewa vifaa vya ufundi stadi na Kanda ya Dar es Salaam ya Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akikabidhiwa Risala ya Atamizi ya Orasika-Tandika jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vijana wa Atamizi ya Orasika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kanda wa chuo VETA, Habibu Bukko akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ufundi kwa Atamizi ya Orasika-Tandika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Vifaa vya ufundi vilivyotolewa na chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabi baadhi ya vifaa vya ujenzi vijana wa atamizi ya Osarika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe, Viongozi wa chuo cha VETA, wanaatamizi ya Osarika wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment