Sehemu ya Wakimbiaji wa Mbio za Mwenge, wakiwa tayari kuupokea Mwenge huo ulipowasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016. Zaidi ya vijana 40 waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya Madawa ya kulevwa wanalelewa katika kituo hicho.Picha zote na Othman Michuzi - MMG.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge huo, akiongoza mbio hizo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukiwasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016.
Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea kituo hicho Mei 19, 2016.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (kushoto) akimkabidhi Mwenge, Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, wakati wa hafla fupi ya Mwenge huo ulipotembelea kituo chake hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga.






No comments:
Post a Comment