Meneja wa msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura), Hemed Kavu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba radhi wa tanzania kwa video ya wimbo wa Msanii Snura na wimbo wake wa Chura.Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.
Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) awaomba radhi watanzania kwa kufanya video isiyo na maadili ya kitanzania ya wimbo wake wa Chura ameomba radhi watanzania mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.



No comments:
Post a Comment